SASA REAL MADRID YALA JEMBE LA KIBRAZILI KAMA NEYMAR JR

Sasa Kocha wa Real  Madrid Julien Lopertegui anabidi afikirie baada ya kiwango kikali kinachooneshwa na mbrazili Vinicus Junior baada ya maendeleo anayoonesha katika timu ya vijana ya Real  Madrid Castilla baada ya kuwa kuna uwezo wa kufanya mambo hayo katika timu ya wakubwa katika kikosi cha kwanza.

Ana vaa jezi namba 28 katika kikosi cha Real Madrid namba 11 akiwa Castilla

Staili anatumia katika kuucheza mpira ikiwa jitihada za kimwenyewe pamoja na ana uwezo wa kupenyeza katikati ya walinzi akiacha mashabiki vinywa wazi kwa chenga zake za kipekee raha yake si kuucheza mpira bali ana jitihada za kufunga ikiwa alipata bao mbele ya Julien aliyetua katika mechi kuwaangalia vijana wa timu ndogo wakifanya yao.


Alijiunga Real Madrid akitokea Flamengo ya kwao Brazili katika dirisha la majira ya kiangazi juji 25.

Si haki kumlinganisha na Neymar lakini Vinicus hana tofauti kubwa na staa huyo aliyetokea Santos na kutua Barcelona kabda ajavunja rekodi ya usajili ya kwenda PSG anakokupigia kwa sasa.

Hii ni ukweli kwamba klabu ya Real  Madrid haina mchezaji wa staili hii licha ya kuwepo kwa Marco Ansensio labda atumike vizuri ndo ana kuwa na uwezo huo lakini si wa staa huyu wa kibrazili .

Castilla sio sehemu pa soka la staa kwani si sehemu itakayompa usumbufu huyu lakini ana pewa nafasi ya kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza lakini hapewi nagasi kabisa ya kusafiri na kikosi cha Real Madrid Lopertegui amekuwa mtulivu na wachezaji aliowasaini pia akimvutia pumzi Vinicus.

Raisi Fiorentino Perez na timu ya maskauti wameridhika na kiwango cha kijana huyu na wana imani ndo mda mwafaka wa kushangaza dunia kwa kiwango chake lakini tatizo kwa Vinisus ni kuwa kocha Julen anajua ilivyo shida kuwa uwanjani na kikosi kilichokuwa kina mtegemea Ronaldo kumtumia kinda huyu kwake ni kama bahati nasibu ana presha ndo maana mpaka sasa hatumii wachezaji waliosajiliwa lakini ana hitaji kumuamini huyu mbrazili.

Katika picha waliyoipiga ya timu nzima hawajamuacha mbali kinda huyo wakionesha nia ya kumtumia katika siku za mbeleni.

Makala na Prosper Barthalomew (M.O).

Simu:+255716243875.

Maoni