PREVIEW : REAL MADRID vc BARCELONA

Kati ya mechi inayoangaliwa  na watu wengi duniani uwezi kusahau kutamka neno "el clasico" yaani mchezo kati ya Real Madrid na Barcelona klabu kogwe za soka Duniani zinakutana  mchana wa saa nane na nusu mda wa afrika mashariki.

MAKOCHA NA REKODI ZA EL CLASICO;
Zidane katika mechi 5 alizoongoza Real Madrid kukutana na Barcelona kashinda 3 , kapoteza 1 , na kasuluhu 1.

Erneste Valdere kama kocha wa Barcelona kakutana na Real Madrid mara 2 katika mashindano makubwa yote akicharazwa msimu huu . Bado ajapata ushindi dhidi ya Real Madrid katika El classico bado anatafuta ushindi wake wa kwanza.

Tukiunganisha na ile iliyofanyika nje ya ardhi ya Barcelona basi Valdere alishinda 3-2 .

MATAJI NANI MBABE?
katika mataji klabu hizi hushiriki mashindano makuu matatu ambayo yote nitatoa takwimu zao .

Laliga Santander;
Katika mchezo wanaokutana ni wa  laliga katika mataji bigwa mtetezi namaanisha Los blacos wanawakilisha mji mkuu wa Hispania wakiwa na mataji 33 na huku Wacatulunha Barcelona wana mataji 24 tofauti ya mataji 9

Copa de rey:
Ni zamu ya wacantalunha kuwakimbiza wenzao baada ya kubeba mara tatu mfululizo yaani ha-trick mabigwa hawa watetezi wa kombe hili wwmebeba mara 29 na Los Blancos wamebeba mara 19 yaani tofauti mara 10.

Ligi ya mabigwa ulaya (UCL):
katika ligi ya mabigwa ulaya wababe wa jiji la Madrid mji mkuu wa Hispania ndo wanaongoza si tu kwa Barcelona yaani mpaka kwa klabu nyingine zote barani ulaya wana mataji 12 na Barcelona wana 5 tu .

Uchambuzi : Klabu ya Barcelona imeipita klabu ya Real Madrid kwa alama 11 ikiwa Real Madrid wajacheza mchezo mmoja ina maana kama Real Madrid watafugwa basi Barcelona atakuwa na nafasi kubwa ya kuongeza kikombe kabatini .

Lionel Messi baada ya kukosa magoli mengi katika mchezo dhidi ya Deportivo la Coruna atakuwa mkali kutafuta goli kuweka kumpiku mpinzani wake mwaka 2017 Christiano Ronaldo  kafunga goli 4 tu katika laliga msimu huu ikiwa ameanza vibaya sana kuokoa maneno madogo madogo yanayoongolewa mtaani atatafuta kuwaadhibu wapinzani wake Barcelona yenye Lionel messi yaani mpinzani wake wa  nguvu.
Christian Ronaldo ametulia laliga misimu 9 na ni msimu mbaya zaidi katika maisha yake laliga .
Lionel Messi anaongoza wafungaji bora akiwa na magoli 14 msimu huu.

Lionel Messi alipofunga goli la ushindi dhidi ya Real Madrid alivua jezi na kuwaonesha mashabiki wa Real Madrid goli lake la 500 la klabu alololifungia uwanjani Santiargo Bernabeu .

Christano Robalno hakufuarahia nae alipofunga uwanjani Nou camp katika Spanish super cup alionesha nae jezi kwa mashabiki wa Barcelona ili kuwaumiza kwa hiyo wanafanyiana kuona nani ni mbabe .

Lionel Messi ana magoli 363 katika ligi kuu hispania ikiwa zaidi ya mchezaji yoyote katika historia ya ligi hiyo .
Christiano Ronaldo ana magoli 286 yaani atatafuta kuifikia rekodi ya mdogo ake Lionel Messi.

Barcelona ijafugwa na timu yoyote laliga msimu huu Real Madrid anatafuta kumfunga ili kuwa timu ya kwanza Hispania kumfunga.

makala na Prosper Bartholomew.
simu :/ +255716243875.
Barua Pepe :/ barthaprosper@gmail.com

Maoni