SIMBA YA MATUKIO

Simba sports club, ni kati ya klabu kongwe hapa nchini lakin juzi usiku iliweka rekodi ya aibu kwa bingwa mtetezi kutolewa katika hatua ya mwanzo kabisa ya kombe la shirikisho la Azam. Hii ni muendelezo wa matukio mbalimbali ya ajabu yanoyoendelea kujenga historia ya soka kwa ujumla. Matukio ya kihistoria mara nyingine hujengwa kwa kujituma au hata kwa uzembe. Klabu ya mbeya city ni klabu ambayo ilipanda daraja na kumaliza msimu wa kwanza wakishika nafasi ya tatu hio nayo ilikua historia kwa ndugu zangu wanyakyusa. Msimu huo ni msimu ambao simba ilimaliza katika nafasi ya nne, sema kiuzury ilitoa mfungaji bora Amiss Tambwe. Simba waliweka tena rekodi ya kumtema mshambuliaj aliyekua mfungaji bora msimu wa nyuma na kumuacha akadondokea kwenye mikono ya yanga ambayo ilimuamin na kwel akamaliza kama mfungaji bora akiwa na yanga. Klabu hii ina msemo wa kujitamba ukisema "THIS IS SIMBA",  Simba kwa sasa inaongoza ligi kuu vodacom ikiwa juu ya yanga na azam. Waliweza kufika huko kwa msaada wa wachezaj na benchi la ufundi kwa ujumla. Benchi hilo lilikua likiongozwa na Joseph Omog , kocha ambae msimu wake wa kwanza kama kocha mkuu wa Azam fc. Alifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu bara. Simba ilipitia vyema CV ya kocha huyo ambaye ashawah kuwa kocha msaidiz wa timu ya ivory coast na kwenda nayo AFCON ya 2010 wakamuamin na wakaona atafaa kuiendesha timu hio yenye maskani yake msimbazi. Mwaka 2016 wakat wa kuanza msimu wa 2016/2017, simba ilimkabidhi kibarua hicho kocha Omog na omog mwenyea aliahid kutwaa kombe katika msimu huo. Mwaka 2017, mwezi wa tano, simba ilishuka katika dimba la Jamhuri Dodoma kuchuana na Mbao fc katika fainali ya Azam Sports Federation Cup,  kocha omog akafanikiwa kutimiza ahadi yake na kufanikiwa kutwaa Ubingwa huo pale mbele ya mashabiki watani zangu wagogo, na kurudisha uhai wa simba uliopotea kwa misimu minne. Simba imemtimua kocha Omog kwa sababu ameshindwa kutetea ubingwa huo katika hatua ya mwanzo kabisa, je kocha huyo hakustahili kuongoza simba msimu huu?, na kama kwel hakustahili mbona ameiacha simba ikiwa kileleni katika msimamo wa VPL msimu huu ?, je hii haioneshi kwamba alikua anaenda kuchukua ubingwa wa VPL?, Jose Mourinho msimu uliopita alivyoona moto wa konte , akajisalimisha na kukazania katika kombe la. Europa ambalo alifanikiwa kulitwaa na kuifanya manchester united kushiriki uefa msimu huu. Kwani Simba Ilitaka Omog Afanyaje?, Simba ambayo sasa ivi inaelekea katika mfumo wa kisasa wa uendeshaji, walitaka kocha omog afanyaje?,  Narudia kauli yangu ya mwanzo, kuna historia zinaandikwa kwa kujituma au kwa uzembe, simba kumtimua kocha wao  ni kuandika historia kwa uzembe , Kaka yangu Haji Manara anasema Philosophy ya omog haina mafanikio wanayoyataka, nauliza swali, je omog angeipasua Green warriors 5-0, angefukuzwa?, ama kwel!!! "THIS IS SIMBA"

Makala na: MC RUGAMBWA
simu :/+255629546461

Maoni