MAKALA: MIAKA (70) YA SANTIAGO BERNABEU , HESHIMA YAKE HII HAPA

Uwanja wenye hadhi na historia Santiago Bernabeu unatimiza miaka 70 tengia uwanze kutumika mnamo mwaka 1947.

Uwanja huo ulijegwa miaka miwili kuanzia mwaka 1945 mpaka 1947 na ulifunguliwa rasmi tarehe 14 decemba 1947 katika mchezo ulihohusisha klabu ya Real Madrid dhidi ya klabu ya Ureno Os Beleneases wenyeji walishinda kwa mabao 3 kwa 1 mchezaji wa kwanza kufunga goli alikuwa Sabino Barinaga.

Uwanja huu pedwa jijini Madrid unaingiza watu 81,044 lakini haitabiriki kwani utawala wanaongeza na kupunguza idadi hiyo ,Ulipofunguliwa ulikuwa unaingiza watu 75,000 ,miaka ya 1950 ulikuwa unabeba mpaka watu 125,000 ,miaka ya 1980 ulikuwa umepunguzwa na kombe la dunia mpaka 98,000 ulishushwa zaidi na matukio ya vifo vya mshabiki uwanjani hasa Uingereza walioweka jinsi viwanja viwepo na miaka ya 1990 na kuingiza watu 75,328.

Kikao cha kamati ya Real Madrid mkutano mkuu wa tarehe nne mosi 1955 uliamua kuupa jina Santiargo Bernabeu kwa mchango aliokuwa anautoa mchezaji  na Raisi wa klabu hiyo kwa miaka 36 Santiargo Bernabeu de Yeste

Klabu ya Real Madrid ilianzishwa mnamo tarehe 6 machi 1902

Uwanja huo umealika fainali ya klabu bigwa ulaya mara nne ikiwa 1957,1969,1986,2010.

Katika ngazi za kitaifa hauko nyuma kama tunavyozani kwani imealika mashindano mbalimbali ;
Katika kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 1964 ulialika fainali , na
pia katika kombe la dunia la mwaka 1982 fainali kati ya Italia na Ujerumani magharibi na kuwa uwanja wa kwanza kualika mashindano hayo mawili makubwa katika historia.

Santiago Bernabeu de Yeste alizaliwa 8 juni 1895 na kufariki tarehe 2 juni 1978.

Aliitumikia klabu hii katika michezo 50 na kufunga magoli 46 .kuanzia mwaka 1911 mpaka 1927.
Alipostaafu soka alikuwa mkurugenzi wa soka klabuni hapo mwaka 1927 mpaka 1933 na kuwa makamu wa kocha 1933 mpaka 36 kisha kupumzika na kurudi kama raisi wa klabu kuanzia 1943 mpaka 1978

Makala na Prosper Bartholomew .
simu :/+255716243875 (whatsapp).
barua pepe:/barthaprosper@gmail.com (email)

Maoni