TIMU ZENYE THAMANI KUBWA KATIKA SOKA NA TIMU ZINAVYOPIGA MPUNGA-2

Timu zenye thamani kubwa duniani ndo tutakazoziongelea leo mathalani za soka.


Pichani:Lukaku na Sanchez wakishangilia moja ya bao alilofunga Lukaku msimu ulioisha katika ligi kuu uingereza.

Zifuatazo ni timu zenye thamani kubwa katika soka timu ya kwanza ni Dallas  cowboys wanatengeneza kiasi cha dola za kimarekani milioni 350,Manchester United $254M, New England patriots $247M,Arsenal $178M, Washington Redskins $145M,Haustons  Texans $141M, Tottenham Hotspur $141M, New York Knicks $140M, Los Angeles Lakers $136M, Manchester city $ 135M.

(TANGAZO) "TUNATANGAZA MATANGAZO YOTE PICHA ,YA VIDEO ISIYOZIDI DAKIKA MOJA NA NUSU,NA MANENO PIA KWA BEI RAHISI SANA HASA KIPINDI HIKI CHA KOMBE LA DUNIA SIKU MARA TATU NA BONUSI YA KUTANGAZWA KWA SOCIAL MEDIA ZETU ZOTE WASILIANA NASI KUPITIA 0716243875"


Hizo hapo juu hizi thamani hazijulishwa na mapato,uuzaji na ununuzi wa wachezaji,na ushuru.

Lakini timu tatu tu Ulaya zinajikuta katika orodha ya timu tajiri ulimwenguni huenda pakatokea mabadiliko maana Ujerumani klabu haziruhusiwi kumilikiwa au ununuzi wa hisa kwa mtu asuye ujerumani.

Zifuatazo ni timu zenye thamani duniani kwa sasa na mwaka 2018.Dallas  cowboys wanazidi kungara wakiwa na thamani ya kitita cha bilioni 4.80 za kimarekani, Manchester United $4.12 B,Real Madrid $ 4.09 B, Barcelona $ 4.06 B, New York Yankees $ 4.00 B, New England Patriots $ 3.70 B, New  York Knicks $ 3.60 B, Los Angeles Lakers $ 3.30 B, New  York Giants $ 3.30 B, Golden State warriors $ 3.10 B, Washington Redskins $ 3.10 B.

Katika soka urushaji wa matangazo ya michezo inaongezea timu pato na kukuza uchumi wa vilabu:katika ligi kuu uingereza kuna vyombo vy habari vimepata hofu kutokana na mkataba wa Amazon na ligi kuu uingereza.

Zifuatazo ni orodha ya ligi na mapato wanayopokea kutoka kwa urushaji na sheria za matangazo ya urushaji wa michezo ya ligi hizo; 

Ligi kuu uingereza inaongoza ikiwa kwa msimu vyombo vya habari vya ndani vinampa dola za kimarekani 2,990 na nje ni 1,290 jumla inakuja dola za kimarekani 4, 280 milioni ambazo timu hupokea. Hii ni kwa mwaka 2017 mpaka 2020.

Bundesliga ama ligi kuu Ujerumani wanapokea kitita cha dola za kimarekani 1,366 kwa ndani na nje 283 dola na jumla kwa msimu ni dola za  kimarekani milioni 1,649 hii ni kwa mwaka 2018-2021.

Serie A ama ligi kuu Italia wanapiga mpunga wa ndani dola 1,111 na nje dola 219 na jumla ni kitita cha dola za  kimarekani 1,330 milioni. Hii n kwa mwaka 2016 mpaka 2018.

Laliga almaarufu kama ligi kuu nchini Hispania nayo inapokea kitita cha dola za kimarekani kwa ndani 1,040 na nje dola 285 ambapo jumla inakuja dola za  kimarekani 1,325 milioni.Hii ni kwa mwaka 2017 na 2019

ligue 1 inaitwa ligi kuu Ufaransa nayo inapiga kitita cha dola za kimarekani za ndani 856 na nje 94 jumla inakuja dola za kimarekani milioni 950.Kwa mwaka 2017 na 2020.

Makala na Prosper Barthalomew.

Simu:+255716243875.


Maoni