TIMU TAJIRI ZAIDI ULIMWENGUNI KWA MWAKA 2018

TIMU TAJIRI DUNIANI-MAKALA -1

Kutokana na gazeti au jarida la Forbes Manchester United imeendelea kushika usukani kwa kuwa timu ghali na tajiri ulimwenguni wakiwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 4.12 kutoka dola 3.69 mwaka uliopita licha ya kutotwaa taji lolote msimu ulioisha.


Tukitoka kwa Manchester United tunaenda Hispania ambapo Real Madrid anashika nafasi kwa kuwa na thamani ya dola za kimarekani 4.09 bilioni anafuatiliwa na Barcelona wenye thamani ya 4.06 bilioni dola za kimarekani.

Tukiachana na hii ya tatu bora tuangalie timu zinazopopata pesa ndefu kwa kutumia Viwanja na udhamini katika jezi.Barcelona anaongoza kwa kuingiza kitita cha dola 247milioni,Manchester United dola 202 milioni,Real Madrid dola 200 milioni,Chelsea 135$M,Bayern Munich 121$M,PSG 100$M,Arsenal 94$M,Liverpool 92$M, Manchester city anatufungia akiwa anapokea 78$M.

Timu na klabu vigogo vinapigana sana kucheza ligi ya mabigwa Ulaya ndo nafasi nyingine ya kuokota pesa za uendeshaji wa vilabu hivi na utawala katika soko la wachezaji ifuatayo ni mpunga ulivyookota Madrid akiwa anajipakulia kwa mara ya tatu mfululizo. Real Madrid akipokea 102$M,As Roma 97$M,Juventus 92$M, Bayern Munich 84$M,Liverpool 79$M, Chelsea 75$M, Manchester city 73$M,PSG 72$M,Spurs 71$M,akishikilia mkia Barcelona 69$M.

Itaendelea.....

Usikose kufuatilia makala hii.

Makala na Prosper Barthalomew.

Simu:+255716243875.

Maoni