SARRI ATETA KUHUSU HAZARD

Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri amekiri ya kuwa kiungo wake nahodha wa Ubeligiji Edern Hazard amemwambia ana uwezo wa kufunga mabao 40 ndani ya msimu mmoja.

Hazard alifunga hatrick dhidi ya Cardiff juzi jumamosi kufikisha mabao matano katika mechi tano za msimu huu.


Edern Hazard: mabao 5 katika mechi 5 za kwanza ikiwa hatrick yake tangu mwaka 2011 dhidi ya Newcastle katika ligi kuu Ungereza

Mfungaji bora wa msimu uliopita alikuwa mshambuliaji wa Misri Mohhamed Salah akiwa na mabao 32 huku wa pili mshambuliaji mwingereza Harry Kane na mabao 30.

Hazard magoli mengi ndani ya msimu mmoja ilikuwa msimu wa 2011-12 ligue 1 magoli 20 akiwa Lille na Kocha wake ana imani atafanya mara mbili zaidi kwa kiungo huyo wa miaka 27 kwa sasa.

  1. CHELSEA 4-1 GARDIFF CITY 

Alipoulizwa kuhusu Hazard kama aliafikia alisema "kama umeshuhudia mchezo wa leo basi ina maana sawa"

Kocha wa Cardiff alisema Chelsea watapata tabu sana katika ulinzi wakikutana na timu za juu msimu huu kwani wako dhaifu sana baada ya kuruhusu mashambulizi hatari pamoja na goli lilofugwa na Bamba kutoka katika mpira uliokufa.

  1. WEST HAM UNITED vc CHELSEA  (15:30 mchana)

Sarri alikiri timu yake kweli ni dhaifu katika ulinzi na watajitahidi kusuluhisha mapema tatizo hilo.


Habari na Prosper Barthalomew (M.O)

Maoni