RONALDO MPYA REAL MADRID


Gareth Bale ni mchezaji wa klabu ya Real  Madrid na timu ya taifa ya Wales alisajiliwa kutokea Totenham Hotspurs kwa dau la pauni 86 milioni akiwa alianza kucheza nafasi ya beki wa kushoto mpaka mshambuliaji wa pembeni akiwa hapo hapo Spurs.

Klabu ya Real  Madrid inatarajia kucheza michezo 7 katika idadi ya siku 21 ndani ya mwezi huu wa 9 ambako ligi ya mabigwa Ulaya inarejea.

Lakini baada ya kuondoka kwa Christiano Ronaldo tulifikiri klabu ingepotea lakini kumekuwa tofauti baada ya klabu hii kupata ushindi katika michezo yote na suluhu moja dhidi ya Atletico Bilbao msimu huu wa 2018 -19 wakiwa wameingia wavuni michezo yao yote.

Lakini siri ya mafanikio haya si mwingine ni Gareth Bale ambaye amefunga mabao kumi kwa timu ya taifa na klabu

Siri ya Bale kuwa moto ni baada ya kuwa fiti kimwili na kitimamu na ni mwaka tangu arejee katika majeraha cha kumvutia ni kupewa muda mwingi na Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya uhispania Julien Lopertegui.

Gareth Bale ana nafasi ya kuwa staa wa klabu kubwa duniani kama akiendelea kuonyesha moto wake alioanza nao huku akiwa na nafasi ya kuwa mrithi sahihi wa mshambuliaji hatari wa Juventus Christiano Ronaldo.

Real Madrid walipata suluhu  ya bao 1-1 baada ya Isco Alaricon kuwasawazishia bao uwanjani Estadio San memes dhidi ya Athetico Bilbao wakiwa wamerejea katika shughuli za kimataifa.

Makala na Prosper Bartholomew (M.O)

Maoni