RONALDO AANZA KUNUSA NUSA

Mshambuliaji hatari langoni pa adui Christiano Ronaldo kafunga bao lake la kwanza katika klabu ya Juventus huku akiongeza la pili baadaye dhidi ya Saussolo dimbani Juventus.

Ronaldo alianza maisha vibaya Italia baada ya kuambulia pa tupu katika michezo mitatu yake ya kwanza ya awali katika ligi kuu nchini humo.


Christiano Ronaldo:akishangilia bao lake la kwanza katika jezi ya Juventus.

Huku Ronaldo akifunga mara mbili lakini amepoteza baadhi ya nafasi ambazo zilikuwa zina uwezo wa kumzawadia hatrick hivi leo.

  1. JUVENTUS 2-1 SAUSSOLO C.Ronaldo (2 goals JUV) -Boubacar (SAU)

Sasa Mnganganizi huyo wa kinyanganyiro cha mchezaji bora wa FIFA (the best) amefikisha idadi ya mabao 400 katika ligi ambazo amezichezea katika klabu za Sporting CP,Manchester United,Real Madrid na sasa Juventus.

Wasiliana na NBA VISUAL Kupata picha kali zinazongaa wasiliana nao kupitia mitandao yote ya kijamii.Bei poa tu...!!!

Katika ukuransa mwingine akiwa Sporting alitumia michezo 3 mpaka kupata bao,Manchester United michezo 10 ,Real Madrid 1, na sasa kibibi kizee cha Turini katumia michezo 4 kabda hajajikuta wavuni mchana wa leo.

Alitua Turin akiwa ametokea Real Madrid kwa ada ya pauni 105 milioni alikoshinda mataji matatu mtawalia ya ligi ya mabigwa Ulaya ikiwa ni matano mataji ya ubigwa ametwaa ya ligi hiyo 1 Manchester United na jingine hapo  na mchezaji wa dunia mara tano kwa nahodha huyo wa kikosi cha Ureno kilichoishia katika nafasi ya 16 bora katika kombe la dunia.

Makala na Prosper Barthalomew (M.O).

Maoni