TETESI ZA SOKA NA TAARIFA ZA USAJILI JUMAMOSI

Mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfred Zaha amekataa mshaara wa pauni 120K kwa wiki.Muivoricosti huyu anawidwa na klabu za Totenham,Everton na Dortmund.


Gianfranco Zola ameiambia klabu yake ya zamani Chelsea ifanye haraka kusuluhuisha tatizo la ukocha mapema huku akikataa tetesi za kurudi klabuni Chelsea kama kocha msaidizi iwapo Sarri atapewa kibarua hapo.

Arsenal wanatarajia kukamilisha usajili wa kiungo Mruguayi Lucas Torreira baada ya kuafikia na klabu ya Italia ya Sampodoria kuhusu usajili huo.

Liverpool wana taka kumsajili Muargentina Paulo Dybala. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Parelmo amekuwa hatambui hatima yake klabuni hapo siku zichache zijazo hasa kipindi hiki Ronaldo anatajwa huko Turin.


West ham inataka kumsajili Dimitri Payet tena klabuni hapo kutokea Olympic Marseille ambapo wanataka kumuuza mshambuliaji huyo,Payet aliitumikia West ham kuanzia 2015 mpaka 2017 januari ambapo alikuwa tishio kwa vigogo pindi alivyokutana nao kabda hajaamua kurudi tena Marseille.

Manchester United wanatarajia kujiweka vizuri na kuandaa kuvunja benki kwa kushutukiza kwa Mshambuliaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo ambaye anatajwa sana na bibi kizee wa Turin Juventus.


Gig Buffon amesaini mkataba wa mwaka mmoja klabuni PSG ya Ufaransa akitokea Juventus kwa usajili wa bure inatarajiwa amekuwa akisaka saka taji la ligi ya mabigwa Ulaya na sasa ameamua kutupia karata zake tena Ufaransa.

Arsenal wako katika maongezi na kiungo Mfaransa Steve N'zonzi ambaye anakipigia Sevilla na kocha Unai Enermy ameshafanya nae kazi klabuni Sevilla hapo awali sasa ana taka kuungana na kiungo huyo anayeitumikia timu ya taifa kwa sasa huko Urusi.


Klabu ya Wolves ambayo ndo imepanda daraja katika ligi kuu Uingereza kwa sasa wana msaka na wamewasilisha ofa ya pauni 16 milioni kwa Manchester city kwa kumtaka kinda wake Oleksand Zinchenko ambaye amecheza mara 16 msimu ulioisha huku akionesha kiwango kikubwa baada ya kumaliza mkopo wa PSV msimu uliopita wa 2016-17.

Stoke city wanataka kumtoa kwa mkopo Xhedraq Shaqiri kwa klabu yoyote lakini si dili la moja kwa moja kama inavyotarajiwa kuwa.

Liverpool wanahusishwa na Mswizi huyo mzaliwa wa Kostovo.

USAJILI na Prosper Barthalomew.

Simu:+255716243875.

Maoni