TAARIFA ZA USAJILI NA TETESI ZA SOKA JUMATATU

Eden Hazard ni chaguo la tatu kama Real Madrid itafeli kumsajili Neymar na Kylian Mbappe kutoka PSG kama warithi wa Christiano Ronaldo.Hazard huenda akawa anasapoti mazungumzo hayo kama ofa ikiwasilishwa.


Klabu ya Arsenal imekubaliana na Lorrient kutoa pauni 8 millioni kumchukua kinda aliyeko chini ya miaka 21 Matteo Guendouzi klabu za Spurs na Man city walisaka saini yake.

Lucas Torreira anatarajiwa kutua mda wowote London kwa ajili ya vipimo vya afya huku kukiwa amna makubaliano binafsi lakini haitakuwa shida.Arsenal wanatarajia kuipa Sampodoria pauni 26 millioni.Usajili huo unatarajia kufanyika mda wowote kuanzia sasa.


Klabu ya Real Sociaded wanaweza wakapata saini ya Mhispaniola Nacho Monreal ambaye kwa sasa Arsenal wanataka kumpiga bei , Hana mkataba unaokamilika mwaka 2019 katika majira ya kiangazi.

Klabu ya Everton ina angalia uwezekano wa kupata saini ya Emil Forsberg kutoka RB Leipzig Kocha Marco Silva anataka vijana kutumikia klabu hiyo baada ya Wayne Rooney kuondoka.

Klabu ya Manchester United imeanza kummezea mate na kuanza mazungumzo kumtafuta Mmexico Lazano anayekipigia PSV ya Uholanzi.


Klabu ya Southampton imeingia makubaliano ya mlinzi wa kati Jannik Vestergard na klabu ya Borrusia Monchegdbach dau la usajili ni pauni 18 millioni.

Kiungo wa klabu ya Barcelona Paulinho amerejea china kwa mkopo wa msimu mzima katika klabu yake ya awali ya Guangzhou Evergrande inayoshiriki ligi kuu China kukiwa na kipengele cha usajili wa moja kwa moja.

Klabu ya PSG imeripotiwa iko tayari kutoa kiasi cha pauni 270 milioni kwa ajili ya kiungo Mbrazili Philiphe Countinho.Ijulikane tu hawa jamaa hawashidwi kwani walimvuta Neymarjr kwa pauni 198 milioni sasa wana mpango huo mezani cha kufikia si makubalano kwani Barca hukaza vichwa na kuweka release clause ambayo haina upingamizo kama mchezaji akitaka kuama.Lakini Countinho alikuwa an a ndoto ya kuchezea Barcelona na si rahisi kukubali kuondoka katika malengo yake.Ni miezi 6 tangu atue Barcelona akitokea Liverpool,Usajili huo una hamasishwa ili Neymar apate raha.


USAJILI na Prosper Barthalomew.

SIMU:+255716243875.

Barua pepe: barthaprosper@gmail.com.

Maoni