TAARIFA ZA USAJILI NA TETESI ZA SOKA JUMANNE

Klabu ya Real Madrid imekataa kwa nguvu uvumi wa kuweka ofa mezani ya kumtwaa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazili anayekipigia PSG ya Ufaransa NeymarJR ambapo inakadiriwa kitita cha zaidi ya pauni 200 milioni huku wakisema klabu haijafanya hivyo. Klabu ya Real Madrid imeamua kutoa taarifa wakisema chombo cha habari cha Hispania TVE wamesema taarifa hizo wakati hawajauliza klabu husika.


Mfaransa Steven N'zonzi amewasilisha ombi la kuomba kuondoka klabuni Sevilla ambapo amekuwa akihusishwa kuhama klabuni hapo na sasa anaangalia uwezekano wa kujiunga na klabu ya Arsenal ya ligi kuu Uingereza.


Klabu ya Swansea City hawajui muafaka wa mlinzi wao wa kati Alfie Mawson kama hatabaki klabuni hapo baada ya ofa mbalimbali kuwasilishwa na vilabu mbalimbali katika ligi kuu Uingereza.


Klabu ya Inter Milan imetangaza kumsajili Kwando Asamaoh kutokea Juventus kwa usajili wa bure .Mghana huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu huku akiwa mtu wa sita kusajiliwa na Inter Milan katika usajili huu wa majira ya kiangazi.

Klabu ya Chelsea inataka kumsajili Allison ama Kasper Schaschmel kama Courtous hatataka kwenda kujiunga na Los Blancos wanaomuwinda kwa udhi na uvumba katika suala la Kasper klabu ya Roma nayo imeweka mkono.

Ryard Mahrez ajaanza mazoezi na klabu ya Leicester city huku akiwa na mazungumzo na klabu ya Manchester city kuhusu kusaini kwa mabigwa hao,Januari alikuwa karibu kutua kwa Citzens kabda ya dili lake kufeli mda wa mwisho wa usajili.


Arsenal walikamilisha kumsajili mgriki Sokratis kutokea Dortmund jana jioni amejiunga kwa bei ambayo haijawekwa hadharani huku akitia mkataba wa miaka mitano katika klabu ya Arsenal atavaa jezi namba 5 mgongoni.


TAARIFA ZA USAJILI NA TETESI ZA SOKA NA :PROSPER BARTHOLOMEW.

Maoni