TAARIFA ZA USAJILI NA TETESI ZA SOKA JUMATATU

Klabu za Liverpool na Arsenal zimeripotiwa kukaza buti kwa ajili ya kumnasa kiungo wa Sporting CP Gelson Martins.Wakala wa kiungo huyo wa miaka 23 amesema na kuthibitisha ya kuwa mchezaji huyo hawezi kujiunga na klabu ya Benfica inayommezea mate kwa karibu akiacha milango wazi kwa klabu za ligi kuu Uingereza.


Klabu ya Ajax inataka kumrudisha beki wao wa zamani Daley Blind ambaye alijiunga na mashetani wekundu mwaka 2014 huku akipata nafasi chini ya kocha Louis Van Gaal, kwa sasa imekuwa tofauti tangu atue Jose Mourhino klabuni hapo mwaka 2016 msimu ulioisha alianza mechi 7 tu za ligi kuu Uingereza.


Klabu ya Arsenal inarudi Argentina kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kumtwaa kinda aliyepata nafasi kubwa katika kikosi cha Argentina Christian Pavon kama mrithi wa muda mrefu wa Alexis Sanchez lakini januari walikataliwa ofa ya pauni 26 na Bocca Juniors lakini wana moyo wa kumtwaa licha ya kuwa na miaka 4 katika mkataba wake wa sasa na klabu hiyo ya Argentina.


Kiungo Mfaransa Adrien Rabiot (23) wakala wake amekutana na wawakilishi kutoka vilabu vya Juventus,Manchester United na Manchester city kuhusu kupata huduma yake kwa sasa amebakiza miezi 12 katika mkataba wake wa sasa na mabigwa wa Ufaransa PSG.


Arsenal wana weza wakakamilisha usajili wa beki wa Dortmund Sokratis mda wowote kuanzia sasa.

Bayern Munich nao wameingia katika rada za kumwania mshambuliaji wa Manchester United Antonio Martial huku klabu za Spurs na Chelsea zikiwa mstari wa mbele,Bavaria watatakiwa kuvunja beki yao ya kufanya usajili ghali zaidi klabuni hapo kwa pauni 70 milioni.


Jurden Klopp kama hatamkosa chaguo lake la kwanza Allson Becker ataingia katika rada za kumtwaa chaguo la pili la Barcelona Jasper Cillisem ambaye alikuwa Ajax kabda ajatua klabuni hapo mwaka 2016.


Mohhammed Salah ameongeza mkataba wa muda mrefu klabuni Liverpool hivi leo na atakaa kwa muda wa miaka 5 zaidi klabuni hapo .Alicheza michezo 50, na kupika mabao 14 huku akifunga mara 43 kwa msimu wake wa kwanza.


TETESI na TAARIFA ZA USAJILI NA:Prosper Bartholomew.

Simu:+255716243875.


Maoni