SUALA LA RONALDO NA REAL MADRID LIKO HIVI,NA MUELEKEO WAKE

Klabu ya Real Madrid haina mpango wa kumuuza staa wao Christiano Ronaldo,licha ya maneno yanayosambaa mtandaoni na katika vyombo vya habari na wanamsubiria arudi aweze kupokea maagizo kutoka kwa kocha mpya Julien Lopertegui.

Tangia Ureno itolewe katika mashindano ya kombe la dunia sasa ameanza likizo yake ya mwezi mmoja kabda ajarudi klabuni hapo inategemewa atajiunga na kikosi nchini Marekani mwezi ujao ama mwishoni mwa mwezi huu.Mchezo wa kuanza maandalizi ni tarehe moja agusti dhidi ya Manchester United Marekani.


Baada ya mchezaji mwenyewe kusema ataachana na mabigwa hao baada ya fainali ya ligi ya mabigwa ulaya mjini Kiev lakini Real Madrid ilimtumia ofa mpya kukiwa na maongezo mapya katika mshaara na masilahi binafsi lakini Ronaldo hajajibu mpaka sasa na huku klabu ikitegemea kupata majibu mda wowote.

klabu kama klabu bado ina imani Ronaldo atawajibu na kutia saini katika mkataba wake uliongezewa mshaara na wao hawajajipanga kumuuza mwanasoka bora huyo mara tano wa dunia.

Yote ya yote klabu ya Real Madrid haiwezi mruhusu staa huyo bila kipunga cha euro 1000 milioni kutoka katika mkataba wake lakini vilabu vinavyomwania vinaamini wakali hawa wa Santiago Bernabeu hawatampaka mafuta kama hakiwa kinganganizi.

klabu ya  Real Madrid ina amini ya kuwa nyumbani kwa Christiano Ronaldo ni kwao na si sehemu nyingine.

Ni klabu ambayo ameweka historia na ana rekodi ya ufungaji bora kwao.

Na wana imani hawawezi mtoa staa wao kwani ni wa kwao si wa sehemu nyingine.

Ndo maana wana haha kumuongezea maslahi binafisi na kumpa kila atakacho haweze kuendelea kuwatumikia klabuni hapo.

Na wana imani hawana mrithi sokoni kwa sasa.

Kwani chaguo lao la siku zote lilikuwa Mshambuliaji wa kibrazili Neymar JR lakini klabu ya PSG haitaki kabisa kusikia mnongono ama hata kukaa meza moja kumuongelea staa huyo hata iweje.

Makala na Prosper Bartholomew.

Simu:+255716243875.

Barua pepe: barthaprosper@gmail.com.

Maoni