Jose Mourinho: Nini kinachoendelea-ama anataka kuondoka Man Utd?

Mwezi mmoja uliopita wakati Uingereza ilipokuwa ikiwania kufika nusu fainali ya kombe la dunia, huku timu kuu zikijiandaa kwa msimu mpya, mechi ya mwisho ya Manchester United dhidi ya Real Madrid ilikumbwa na maswali chungu nzima.

Gareth Bale atachezeshwa lakini atamchezea nani? Mbali na maandalizi ya msimu huu, hatahivyo Bale sasa anafuraha chungu nzima baada ya mkufunzi mpya wa klabu hiyo Julen Lopetegui kumhakikishia kwamba atamshirikisha katika kikosi chake.

Na huku Man United ikijianda kwa mechi ya siku ya Jumatano , maswali mengi juu ya United bado yanasalia.

Matamshi ya mkufunzi Jose Mourinho katika uwanja wa Michigan nchini Marekani siku ya Jumamosi wakati kikosi chake kilipopoteza 4-1 yalikuwa na uzito mkubwa.

Hivyobasi ni wakati wa kuuliza maswali haya.

Ni nini kinachoendelea na Mourinho na Manchester United?

Kwa nini Mourinho hana raha tena?

Mbele ya kamera ,Mourinho amekuwa mtu ambaye hana raha kwa muda mrefu sasa. Kitu, makovu ya kukabiliana na vyombo vya habari vya Uhispania wakati akiifunza Real madrid yalitokea wakati akiifunza Chelsea mara ya kwanza na mara ya pili.

Chochote kile , Mourinho amebadilika na kuwa mkufunzi ambaye motisha yake imeshuka katika klabu hiyo.

Hatahivyo malalamishi aliyotoa baada ya mechi dhidi ya Liverpool yanaonyesha kocha aliyeshushwa mabega.

Alilalama kuhusu ukosefu wa wachezaji nyota, kiwango cha baadhi ya wachezaji wadogo mbali na kuzungumzia kuhusu malengo yake ya wachezaji wapya ambayo anaona hayataafikiwa , akisema kwamba baadhi ya wachezaji wake wanahudumia majeraha, akawomba wachezaji nyota kurudi matika mazoezi mapema na akahoji ni kwa nini mashabiki wanalipa ili kuona timu yake ikicheza.

Katika mkutano wake na vyombo vya habari uliochapishwa sana na kutangazwa, alimshukuru beki Eric Baily kwa kuingia na kuchukua mahala pake Chris Smalling wikendi, na baadaye kumkashifu raia huyo wa Ivory Coast kukosa uongozi.

Image copyrightGETTY IMAGESJose Mourinho uwanjani Old Trafford

Akizungumza na runinga ya United , alimshutumu nahodha mpya Antonio Valencia kwa kurudi kutoka likizo na kiwango cha chini cha mchezo.

Akiongezea , alishutumu kiwango cha refa ambaye alitoa penalti mbili dhidi ya timu yake.

La muhimu ni je Mourinho ameanza kukasirishwa na mambo haya yote , je anajaribu kuwasilisha picha fulani?

Ama anatafuta sababu za kujiondoa katika lawama baada ya kushindwa vibaya na wapinzani wake katika ligi ya Uingereza Liverpool?

Iwapo sio hayo yote basi ni miongoni mwa mbinu za ukufunzi wake ama anataka kuondoka baada ya miaka mitatu swali ambalo hulikataa kwa haraka anapoulizwa.

Je uhusiano wake na klabu h yo umeharibika?

Kuna majibu mawili ya kile ambacho Mourinho alikifanya siku ya Jumamosi. Mwanzo mtu atajiuliza maswali, na kusema ni tabia yake ama amuonee huruma na hali yake na kusahau.

Hiki ndicho kinachofanywa na idadi kubwa ya viongozi wa klabu hiyo. Hatahivyo raia huyo wa Ureno alitia saini kandarasi mpya mnamo mwezi Januari ambayo iliimarisha mahitaji yake ya kikazi mbali na kumuongezea kandarasi yake hadi mwaka 2020.

Uhusiano kati ya Mourinho na naibu mwenyekiti wake Ed Woodward umesemekana kuwa mzuri sana kati ya wote wawili hivyobasi mpango wowote wa kuwanunua wachezaji wapya ungejadiliwa na kuafikiwa katika mazungumzo yao.

Hivyobasi ni nini ambacho kimebadilika baada ya kukosa kumsajili mchezaji mmoja- swala ambalo limekuwepo misimu miwili iliopita? hayo ni maoni mbadala, na kuna wakuu wengine ambao wameanza kulemea upande huo, je Mourinho anataka kuondoka na huu ndio mpango wa kutaka kujiuzulu?

Kitu ambacho ni wazi , kwa mara ya kwanza katika kazi yake , Mourinho hatakuwa na Rui Faria upande wake msimu huu.

Wawili hao wamekuwa pamoja tangu Mourinho alimpomchagua Faria -mtu anayemtaja kuwa nduguye- akiwa naibu katika klabu ya Uniao Leiria mwaka 2001.

Hatahivyo , msimu uliopita , Faria ambaye alihisi kwamba imekuwa vigumu kuonana na familia yake na kuchoshwa na presha ya kuhusishwa mara kwa mara na mechi za klabu hiyo aliamua kupumzika.

Mourinho ameamua kutoleta mkufunzi mwengine kuchukua mahala pake.

Kupitia Michael Carrick na Kieran McKenna, ameongeza mmoja ya wachezaji ambaye ana uzoefu mwingi wa mchezo huo na alliye na tamaa ya kutaka kujifunza na mtu ambaye sifa yake akiichezea United na Tottenham ni kubwa .

Huku United ikimaliza pointi 19 nyuma ya mabingwa wa ligi Manchester City- ambao meneja wake Pep Guardiola anashindana na Mourinho katika kuwania taji la mkufunzi bora wa kizazi chao- na hawajafanya kitu chochote kuhakikisha kuwa pengo hilo linajazwa, Matamshi ya Mourinho siku ya Jumamosi yanaonekana na wale ambao wamezoea kuondoka kwa makocha kama mwanzo wa kwaheri ya muda mrefu.

Man United iko katika hatari ya kupitwa na wapinzani wao?

Mchezaji muhimu aliyesajiliwa na United kufikia sasa ni kiungo wa kati wa Brazil . Beki mwengine wa kati anatarajiwa, ni nani? hilo halijawekwa wazi.

Hatahivyo wote wawili watakuwa miongoni mwa wachezaji sita ghali ambao United imewahi kununua.

Kati ya wengine wanne, ni mshambuliaji wa Argetnina Angel di Mario ambaye hayuko katika klabu hiyo.

Katika safu ya kati Paul Pogba na mshambuliaji Anthony Martial, wawili hao ambao wamesalia hawajaonyesha mchezo wa kiwango cha juu mara kwa mara.

Mourinho hakuhusika katika kumsaini Martial kutoka Monaco.

Maoni yake ni kwamba mshamuliaji huyo wa Ufaransa hupotea wakati muhimu hivyobasi anataka kumsaini mshambuliaji wa Croatia Ivan Perisic kutoka Inter Milan.

Mkufunzi huyo alihusika katika uhamisho wa Bailey, beki mwenza Victor Lindelof na mshambuliaji Alexis Sanchez -kwa dau la chini ya £100m, wachezaji ambao Bado hawajaleta mabadiliko makubwa katika klabu ya United.

Wakati huohuo haijulikani wapinzani wa United wana mpango gani.

Mchezaji wa pekee aliyesajiliwa na Manchester City msimu huu ni Riyad Mahrez, mshambuliaji ambaye pengine klabu hiyo haimuhitaji. Tottenham haijamsajili mchezaji yeyote.

Mchezaji aliyesajiliwa kwa dau la Juu tangu kuingia kwa mkufunzi mpya katika klabu ya Arsenal ni kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira ambaye uhamisho wake wa £26m, uligharimu nusu ya fedha ilizotoa United kumsaijili Fred.

Chelsea haikumsajili mkufunzi wake mpya hadi baada ya mechi za maandalizi ya msimu mpya zilipoanza.

Kati ya klabu kubwa za Uingereza , ni Liverpool pekee ambayo inaonekana kuwa na mwelekeo mzuri licha ya kwamba wachezaji watatu kati ya wanne iliowasajili hawajacheza katika ligi ya Uingereza.

Hivyobasi, huku ikiwa ni rahisi kuona United ikirudi nyuma, inaweza kuhojiwa kwamba iwapo wachezaji waliosajiliwa na Mourinho wataimarisha mchezo wao hawatakuwa mbali kupata ufanisi.

Je inamaanisha nini kwa msimu wa United?

Katika klabu zote , matokeo yanaweza kubadilisha matarajio ya wengi. Man United inacheza mechi yake ya kwanza ya ligi dhidi ya Leicester mnamo tarehe 10 Agosti.

Mourinho tayari ameangazia vile ambavyo Leicester imejiandaa kwa kuwa ni wachezaji wake wachache walioshiriki katika kombe la dunia nchini Urusi.

Hilo ni kweli. Lakini Jamie Vardy na Harry Magwire waliichezea Uingereza hadi katika mechi ya nusu fainali, Mahrez ameuzwa.

Je wanaweza kuishangaza United siku wa ufunguzi wa ligi kuu? Pengine hapana , mara ya mwisho kwa Leicester kupata ushindi katika uwanja wa Old Trfford ni 1998.

The Foxes huenda walishinda ligi ya Uingereza hivi majuzi ikilinganishwa na United. Baadaye United itaelekea Brighton na baadaye Burnley ambapoo huenda wakashiriki katika mechi hiyo baada ya kushirika kwa mara ya sita katika kombe la Yuropa.

Maoni