Cuadrado akubali kumkabidhi Ronaldo namba saba



Ronaldo amejiunga na Juventus akitokea Real Madrid kwa mkataba wa miaka minne kwa dau euro milioni 100 ambapo zitaongezeka euro milioni 12 katika kipindi cha miaka miwili baadae, hivyo baada ya kusaini ni wazi Ronaldo atatumia jezi yake namba saba ambayo amekuwa akiitumia miaka mingi.

Jezi namba saba kwa Juventus ilikuwa inavaliwa na Juan Cuadrado na baada ya Ronaldo kutangazwa rasmi kujiunga na JuventusCuadrado amekubali kubadili namba ya jezi na kumpa namba 7 Ronaldo “Ni baraka sana kutoa kuliko kupokea”

Maoni