CHRISTIANO RONALDO, NA REAL MADRID ILIYOFELI

Wiki hii inayotarajia kuanza kesho kuna kila dalili mapacha wawili wakatengana yaani Christiano Ronaldo na klabu ya Real Madrid.Baada ya miaka 9 ya mafanikio katika kuta za Santiago Bernabeu sasa inaonekana ni muda muafaka wa mchezaji huyu kuondoka.


Kuondoka kwa staa huyu kutayumbisha klabu bigwa Ulaya na kuchanganya baadhi ya wachezaji wa Real Madrid.

Kila mtu anajua ni ngumu tena kwa mreno huyu kufanya na kufikia malengo ambayo ameyafanya hapa Hispania sehemu nyingine ata kama ni Turin.

Kila mmoja haelewi ni nini hasa kama ni klabu yenyewe ama mchezaji mwenyewe ana tumia nguvu kulazimisha kuama inaonekana ya pili ni kweli mashabiki wanataka asimame aseme mwenyewe.


Ijulikane katika soka amna linaloshindikana kwani Mbrazili Neymar JR mwaka uliopita alituthibitishia.

Nadhani msimu wa 2018 na 19 utakuwa muda mgumu sana ambao ujawai tokea klabu itayumba na kuteseka kucheza bila staa wao wa kutisha.

Kipengele cha mauzo ya mchezaji huyu kinashuka kila siku kutokana na mwoonekano wake sasa kutoka Euro bilioni moja mpaka euro 100 milioni.

Ukweli usiofichika Ronaldo anaondoka Real Madrid kutokana na Raisi wa klabu hiyo mheshimiwa Fiorentino Perez.

Na ilikuwa ndoto yake kustaafu katika kuta za Santiago Bernabeu na ilikuwa kipaumbele chake.

Sababu za kuanza ni ajapewa mkataba wa mshaara mzuri,maslahi na kingine kuhusishwa na Mbrazili Neymar JR ni kitu kilichomuumiza sana.

Kutopata bao dimbani Kiev katika fainali ya ligi ya mabigwa ulaya ilimuuma sana na kumchanganya na kulingana na maneno ya Raisi pia ikawa ndo basi.

Mashabiki na viongozi wa Real  Madrid inaonekana walikuwa wanapenda magoli yanayofugwa badala ya mfungaji mwenyewe ni kila dhahiri jumla ya bao 451 takribani.

Kocha wetu mpya Julien Lopertegui ana ata kauli ya kumsimamisha huyu Mreno akijua msimu ujao atapoteza takribani bao za asilimia 40 au 50 za klabu hiyo. Moyoni mwake akili itachanganyikiwa kama ilivyotokea kwa Valverde msimu uliopita kwa Neymar na hii ya Ronaldo ni kubwa sana.

Ronaldo kawarudishia heshima yote iliyokuwa imebebwa na kuanza kuibwa na huyu Muargentina wa Catalunia Lionel Messi mataji 13 kwa 5 katika ligi ya mabigwa Ulaya ambayo tofauti hiyo ilikuwa kabda Messi ajazuka kuwa staa ndo iko vile vile sasa itapotea ama itapunguzwa.

Ni dhambi kubwa inayofanywa na Fiorentino Perez ana msahau kijana aliyetwaa mataji 16 klabuni hapo.


Raisi kamchoka na sasa ana mtamani Mbrazili NeymarJR kutoka PSG kuliko huyu Mreno Real  Madrid ina uwezo wa kumpa kila kitu lakini Ronaldo si kwa pesa ame dhalilishwa mimi namsapoti kwa si za dharau anazooneshwa na huyu Raisi.Kamuona mabaki sasa ataki kusikia chochote anajifanya anataka abaki lakini ana malengo yake pengine.

UCHAMBUZI na Prosper Barthalomew.

Simu:+255716243875.

Barua pepe: barthaprosper@gmail.com

Maoni