YANGA YA MANJI

Jana siku ya tarehe 10 mwezi wa 6, ilikua ni kikao cha halmashauri kuu na wanachama wa klabu kongwe nchini, Yanga SC. Yanga walihitisha kikao hicho kama ilivyo kawaida yao kwa kila mwaka kuwa na mkutano mkuu, ili kuweza kujadiliana mambo mbali mbali yahusuyo maendeleo ya klabu hio kiuchumi na kimpira zaidi. Mkutano huo ulihudhuriwa na watu wengi , wakiwemo Mawaziri, na pia viongoz mbali mbali wa yanga wa zamani. Mh.Harrison Mwakyembe alikuepo kama mgeni rasmi, pia Waziri Mkuchika hakuacha kuhudhuria kwa sababu yeye ni mnazi wa klabu hio kongwe nchini. 

Pichani:Yusuph Manji akionekana pichani

Moja ya ajenda ya kikao hicho ni kupitia upya ombi la kujiuzulu la mwenyikiti wa yanga, Yusuf Manji. Watu wote kweny hiko kikao walikua wanasubiria ifike muda wa hio ajenda ili wafanye maamuzi sahihi.


Ikumbukwe *yanga ya manji* ni ile yanga ambayo iliogopeka sana ukanda huu wa afrika mashariki na kati, ni yanga ambayo iliunda kikosi kikali kilichopendelea zaidi kucheza kwa mashambulizi na kuwanyanyasa wapinzani wao, ni yanga ambayo imeweza kutwaa ubingwa wa ligi kuu mara tatu mfururizo mbele ya watani zao Simba.


Baada ya Manji kujiuzulu yanga iliyumba kwenye kila sekta, kwanzia uongozi, uchumi wa timu, na hata matokeo ya uwanjani. Je! Kuna mwanachama ambae alikua anawaza kulikubali ombi la manji la kujiuzulu?


Ilivyofika muda wa hio hoja, wanachama wote waliokua wamekaa ndani ya ukimbi huo wa Police Mess oysterbay kwa sauty moja walilikataa ombi hilo na kutaka mwenyekit wao arejee ofisini ili kuikomboa timu hio katika majanga.


Yanga ni ya manji bwana!, na manji peke ake ndo anaweza kukaa pale na kuifanya iwe tishio hapa nchini na kimataifa. Hasara za kuondokwa kwake zimeshaonekana na wanayanga wenyew wamechoka kubezwa na wapinzani wao , wamechoka kuishi bila kombe, kama ilivyokua miaka mitatu iliyopita.


Sambamba na hilo yanga iliunda kamati kwa ajili ya kukamilisha usajili wa nguvu , na kamati hio ipo chini ya Abass Tarimba (mkurugenzi wa sportspesa tz), na waliomo ni wakina Bin khleb na Hussein nyika bila kumsahau Ndama, kwa kamati hio na manji akirudi ofisini basi ile yanga ya zaman itarudi tena ikiwa na moto mpya wa kusaka mafanikio zaidi.

Hio ndo Yanga Ya Manji

Makala na: Rugambwa (infantino)

Simu:0629546461

Maoni