WOSIA KWA WACHEZAJI WA ARGENTINA ,MOURHINO NA ZABALETA WAGONGEA MSUMARI

Argentina hawajawai shinda taji la kombe la dunia tangu mwaka 1986 na kikosi chake cha wachezaji 23 kati yao 15 wana umri uliozidi miaka 30.


"Ni nafasi ya mwisho kwao "Zabaleta alisema

Tangu kupoteza kwenye fainali ya 2014 dhidi ya Wajerumani Argentina wamepoteza fainali mbili za Copa America za 2015,2016.

Nahodha Lionel Messi atakuwa na miaka 35 pale kombe la dunia litafanyika mwaka 2022 pale Quatar ni kati ya wachezaji ambao wana nafasi ya kumaliza maisha yao ya soka la kimataifa bila kombe kwa upande wa Argentina.

Jose Mourhino alisema huu ni wakati wa mwisho kwa Lionel Messi na Christiano Ronaldo kushinda kombe la duniani maana umri utakuwa umewatupa mkono mwaka 2022.

"Ukioana wachezaji wanacheza kombe hili ina maana kubwa kwao,maana ni nafasi yao ya mwisho kwao kufanya kitu na timu ya taifa"Zabaleta ambaye alicheza fainali ya 2014.

Miaka yote ya 1982 na 1986 Argentina walikutana na Wafaransa katika hatua tofauti na kufanikisha kushinda taji hilo la kombe la dunia.

Zabaleta hakuwa na kuficha na kusema ya kuwa licha ya Wafaransa kuwa na wachezaji wazuri bado hawajacheza katika kiwango kilichotegemewa.

Kombe la dunia na Prosper Bartholomew.

Simu:+255716243875.

Barua pepe: barthaprosper@gmail.com





Maoni