Klabu ya Atletico Madrid imewatia saini hapa Urusi baadhi ya wachezaji wake ikiwamo Thomas Lemar wakiwamo mazoezini.
Antonio Graizemann ameongeza mkataba mpaka mwaka 2023 utakaomuweka kusalia klabuni Atletico Madrid,wiki iliyopita alithibitisha ya kuwa ataendelea kusalia klabuni hapo licha ya kuwa windo kuu na klabu ya Barcelona na Manchester United iliyomsaka katika majira ya kiangazi ya mwaka 2017 na kuamua hivi hivi.
Lucas ambaye ni beki mfaransa amekuwa nguzo kuu ya mafanikio klabuni hapa wameamua kumpa ofa na ametia saini mpaka mwaka 2024 majira ya kiangazi hapa kambini Urusi.
Thomas Lemar ametia saini rasmi klabuni Atletico Madrid akiwa bado hapa kambini Ufaransa nchini Urusi ambapo anategemewa kutambulishwa rasmi mashindano yatakapofika tamati.
Habari na Prosper Bartholomew.
Simu:+255716243875
Maoni