VIBENDERA WAPUNGUZIWA KAZI SASA YAZIDI.

Marefa wasaidizi yaani vibendera wameambiwa wakati wa kombe la Dunia wasinyooshe bendera kuonesha kuotea kama kuotea watakuwa hawana nayo uhakika kwani watahudhuria na msaada wa video (VAR) baada ya tukio kutokea eidha goli au kona hata penati.

Urusi itakuwa nchi ya kwanza kufanyika kombe la Dunia na kutumia uamuzi wa msaada wa video yaani (VAR).

"usipoona baadhi ya wasaidizi kutonyoosha vibendera haina maana amekosea "Alisema Collina."kwa sababu atakuwa anaheshimu maagizo ya kuweka kibendera chini"

Muamuzi huyu wa Italia mstaafu Collina alikuwa akihubiria mkutano wa waandishi wa habari wa waamuzi hivi leo jumanne.

Huku akisema inawezekana shambulio husika si la kuotea lakini mwamuzi akakosea na akainyima timu nyingine pengine ambapo kama ilikuwa ya kuotea ingerudiwa na kutoa maamuzi sahihi.

Raisi wa FIFA alitamka rasmi mfumo utatumika katika kombe hili la dunia baada ya kutumiwa na kufanyiwa mazoezi katika ligi za Ujerumani na Italia na pengine katika mashindano ya makombe mbalimbali ulimwenguni.

Kombe la Dunia na Prosper Barthalomew.

simu:+255716243875.

Barua pepe: barthaprosper@gmail.com.

Maoni