Kocha wa Misri Cuper, alikua kajipanga na vijana wake vyema ili kupata ushindi katika mchezo huo. Kikosi cha mafarao wa misri kilikua na wachezaji wengi ambao wanacheza klabu za hapa hapa afrika wakiongozwa na golikipa wao Mohamed El shanawy ambae anadakia klabu ya Al Ahly. Kipa huyu alionesha uwezo wa hali ya juu sana na kuzuia mashambulizi mengi yaliofika eneo lake la kazi kwa kupitia nyota wa kimataifa Luis Suarez na Edison Cavani.
Mechi hio ilikua ni piga nikupige kwa mpaka kipindi cha kwanza kinaisha misri walikua wamepiga shuti moja tuh la kulenga goli. Uruguay walionekana kuwasumbua sana wamsri ila kwa uimara wa kiungo wao kutoka klabu ya arsenal El Neny waliweza kutuliza mashambulizi hayo dimbani. Uruguay ilikua ina wachezaj wazoefu ambao waliweza kusumbua vyema ngome ya wamisri. Wachezaj kama Rodriguez waliongia kipindi cha pili kuongeza mashambulizi, walisumbua sana misri.
Vijana wa misri leo waliweza kuonesha dunia zima kwamba bara la afrika lina ukomavu katika soka na sio wa kudharaulika. Wachezaji walicheza utadhani kama ndo fainali, Watu kama Eghazi na El Shafty walipiga mpira mwingi sana kiasi cha kuwafanya uruguay kuanza kutafuta goli kwa faulo na mashhti ya mbali. Dakika zilivyokua zinayoyoma Luis Suarez alipata shambulizi moja na kushindwa kulifanyia haki. Pia Edison Cavani alifanikiwa kupata nafasi ya kupiga mpira wa adhabu na kugonga besela langoni mwa misri.
Mwisho wa siku bahati haikuwa upande wa afrika na uruguay waliweza kupata mpira wa adhabu eneo karibia na kona na kupiga vyema mpira huo na mchezaji aliyesani mkataba wa miaka mitano na klabu ya Atletico Madrid , Giminez, alifanikiwa kupiga kichwa cha nguvu na kuuzamisha mpira wavuni kwa mafarao hao. Na baada ya dakika chache wamsiri walijaribu kurudisha ila muda haukuwa upande wao na filimbi ya mwsho ikasikika.
Katika kundi hilo Uruguay inaongoza kwa pointi 3 na goli moja. Misri bado ana mechi mbili, je! ataweza kujipanga upya na kupenyeza katika hatua inayofata??
Kutoka Russia
Kombe la Dunia na /Uchambuzi na Rugambwa (infantino)
Mawasiliano 0629546461.
Maoni