Saudia Arabia imekuwa nchi ya kwanza kucheza mechi ya ufunguzi kutoka bara Asia kwingine ni kuwa mchezo huu utakipigwa dimbani Luzhinik mjini Moscow.
Imepita siku 1432 tangu goli la staa wa Ujerumani Mario Gotze kufunga goli la dakika ya nyongeza ni mda mwingine kufungulia na kuandika historia katika vitabu vya Urusi na dunia nzima.
Vikosi vyote vinacheza mchezo huu kukiwa na matokeo mabaya kwa timu zote si Urusi wala Saidia Urusi mara ya mwisho Urusi kushinda ilikuwa mwezi Octoba dhidi ya Korea tangia amecheza michezo saba ajashinda kabda ya mchezo wa leo.
Huko Saudia ajashinda michezo mitatu mtawalia ya kupasha misuli dhidi ya Italia,Peru, na washika taji Ujerumani.
Zote zinataka kufuta rekodi chafu inayowaandama hapa dimbani Luzhinik ,Urusi hajawai shinda mchezo wowote katika kombe la Dunia tangu mwaka 2002 wakati cha kushangaza zaidi Saudia ajawai fanya hivyo tangu 1994 dhidi ya Marekani.
Haijawai tokea mwenyeji wa mashindano akafungwa katika mechi ya ufunguzi,na hii ni kombe la Dunia la 21 tangia mwanzo wake mwaka 1930.
kwa muda wa Afrika Mashariki mchezo utaanza saa 12 kamili jioni.
kombe la Dunia na Prosper Barthalomew.
Maoni