Pande zote zitacheza kwa umakini mkubwa wakijua ya kuwa upande wa Urusi ana mabao matano yakiyoko kabatini na Saudia ana chochote,mchezo huu unatarajiwa kuwa mchezo wa ufunguzi katika siku ya pili hapa mjini Enkaternburg.
Mafarao wamepata tena moyo baada ya kutoshiriki kwa muda mrefu na kusikia habari ya kuumia kwa mshambuliaji wao ambapo taifa nzima liko nyuma yake ana nafasi tena ya kuitumikia timu hiyo Kocha Hector Cluper alikiri jana hapa mjini Enkaternburg watapata huduma ya mshambuliaji huyu wa Liverpool.
Washindi mara mbili Uruguayi wamekuwa wazuri takribani kwa kombe la Dunia chache zilizopita huku 2010 wakimaliza wanne na 2014 kutolewa 16 bora pale Brazili.watakuwa wanafurahia huduma ya washambuliaji pacha wao Luis Suarez na Edsson Cavani ambao huku Ulaya wamekuwa wakiwatoa majasho mabeki mbalimbali.
Katika mchezo wa leo tutaona nani anatamaa ya magoli kati Salah aliyetwaa kiatu cha mfungaji bora ligi kuu Uingereza Edesson Cavani aliyefanya hivyo Ufaransa ama Luiz Suarez anayewashwa mpaka kungata mabeki?
Uruguayi wajawai kushinda mchezo wao wa kwanza wa Kombe la dunia tangu mwaka 1970 tangu hapo wamefugwa 3 na kusuluhu 3 na ni ndani ya miaka 48 je swali linakuja wataweza kufanya chochote?
Kombe la dunia na Prosper Barthalomew.
Maoni