UBELIGIJI INAVYONGATA TARATIBU NA MADHARA MAKUBWA.

Kama kuna timu ya taifa ambayo inatisha kwa kukupigia mashuti mengi katika goli lako basi si kushauri ni Ubeligiji ata hivyo kocha wa Uingereza ashakiri na anahofu na  mchezo huo utakavyomsumbua.

Chini ya kocha wao Roberto Martinez ambaye ndo mwamuzi mkuu ndani ya kikosi hicho anapenda kuchezesha timu yake katika mfumo wa 3-5-2 au ukiugawanya zaidi ni 3-4-1-2 mambo yakiwa si hivyo 3-4-2-1.Hazard huwa nyuma mara nyingi ya washambuliaji Lukaku na Martens au Batshuayi. Au siku nyingine Martens hucheza na Hazard kama namba kumi pacha .


Mabeki hapa hucheza watatu lakini itategemea kama Vincente Kompany kapona au maana alipata jeraa katika mchezo dhidi ya Ureno hapa Vertongen,Kompany na mwingine kama watapangwa hutulia kazi kubwa kumlinda Thibout na kuua mashambulizi ya kushtukiza yanapotokea baina ya pande wanayocheza nayo kumfikia Courtous lazima uwe umejipanga pangika.Kompany hapa ndo kiongozi wao atawaelekeza wenzake ndani ya uwanja na kuwatuliza kwani ana jiamini kwani amecheza michezo migumu sana na mikubwa.

Viungo ndo wanakipa kiburi hiki kikosi katikati anakuwekea Witsel na Kelvin Bruyne ambapo Bruyne anacheza kama kiungo msambazaji na Witsel anacheza soft ukapaji na uchafuaji katikati huko pembeni anakaa Carrasco ambaye anakipiga kama beki winga wa kushoto kulia anacheza beki wa PSG Meunier wote wanafanya kazi moja Carrasco mara ya kwanza alikuwa winga lakini kocha wake wa timu ya taifa anapenda zaidi kumtumia katika nafasi hiyo ndo anakipa kiburi upande huo maana kufunga anajua pasi anajua mashuti ni mzuri grosi nae sasa unakuta mpira ukienda upande wake timu nyingine hua tumbo tujo.

Meunier ashafunga hatrick katika nafasi hiyo  mwaka jana katika mechi ya kufunzu Kombe la  Dunia,nadhani kwanza pembeni unateseka alafu uje kwa yule aliyeipa Manchester city ubigwa na Guardiola akatembea kama mwanaume katika viwanja visivyo vyake tena vikubwa huyu kijana KDB pasi anazipiga vizuri sana na mashambulizi ya kushtukuza ndo usiseme ukute umepandisha timu umkute mpira basi hesabu lukaku au Martens kakutenda bado watamiliki mpira mpaka ujisikie umeshiriki kombe la dunia kwa kukosea wachezaji wako watapumilia mashine watakimbizwa kupigiwa pasi mpaka wachoke wachoke tena.


Washambuliaji kazi yao kukungata na kukumeza taratibu hawanaga haraka sana wanajua lazima utangatika tu namaanisha hawana papara wakiwa na mpira kama zilivyo timu nyingine mpaka Lukaku katulia pale mbele huongozwa vizuri na nahodha Hazard.Lukaku ataambiwa atatii pia Martens atafanya hivyo baadaye watakuingizia Batshuayi na Hazard mdogo kukumalizia kama umebakiza maini na miguu hawa ni simba wasiokuwa na njaa ya haraka lakini lazima wakungate ujiulize ni wewe au.

Ndo maana imepewa pia nafasi ya kutwaa taji hili wakiijumlisha katika timu nne zenye nafasi kubwa ya kucheza nusu fainali.


Tumalizie kwa kusema siri moja iliyoko ndani ya kikosi hicho ni hakina uchoyo hata utakuta Lukaku ana magoli mawili lakini akimuona mwenzake atampa afunge kama akiwa wazi na nafasi. Hazard huwatoka wachezaji wengi lakini humchungulia wapi mwenzake yupo hutoa au kumpa pasi.Si mchezaji mmoja bali wote yote hufunikwa na maneno yanayosema hujituma ndani ya uwanja zaidi ata ya viwango vyao.


Kombe La  Dunia Prosper Barthalomew.

Simu:+255716243875.

Baruapepe: barthaprosper@gmail.com.



Maoni