UBELGIJI WAJITATHIMINI LASIVYO WATAKUFA KIBUDU

Jana mechi za kundi G za kufungua zimeisha huku timu zikioneshana ubabe.


Ubelgiji na Panama,Nafikiri Panama alikuwa bado mgeni na wa hofu kubwa katika mashindano haya makubwa ulimwenguni walijitahidi kuwa bora lakini walijitahidi mpaka kufika kwenye boksi la mmbeligiji ndani ya dakika 45 walilinda vizuri wakimfunika mshambuliaji Romelu Lukaku na wakijitahidi kuzipa nafasi ambazo zingeleta madhara Ubelgiji walikuja kuwa bora kipindi cha pili kwa kutumia mipira ambayo Panama alikuwa anaipotezea na Lukaku akawa bora na kufunga mawili na ndani ya benchi la ufundi lina mkogwe ambaye ni chachu mfaransa Thiery Henry.

Lakini tatizo kubwa lilionekana kwa Ubelgiji kutokuwepo maelewano baina ya Alderwield na Vertongen lakini matatizo yao yatasuluhishwa kwani wana cheza timu moja wanabidi wapewe maelekezo machache baina yao na kuambiwa lakini kwa kouyate Boyata amekuwa safi ametulia nahisi Ubelgiji wanakula matunda ya beki huyu wa Celtic.

Kiungo hasa kwa Bruyne Ubelgiji akikutana na timu kubwa nafasi anayocheza kiungo huyu si yake kwani hana uwezo mkubwa wa kukaba na kazi ya kukapa pale mipira inapopotea ina kuwa ya Witsel ndani ya uwanja na kutafanya Ubelgiji kuwa dhaifu na kutawaliwa katika eneo la kiungo apo atabidi kuua namba 10 moja ambapo ya Martens alafu amlete Dembele ndani au Felaini.

Lasivyo Ubelgiji atatawaliwa mpira eneo la kati na kusababisha kutegemea mashambuluzi ya kushtukiza na huku Bruyne atapotea ndani ya uwanja wanabidi waweke mpango thabiti wa timu ndani ya uwanja hasa kuhusu eneo la kati ambapo kwa michezo ya hivi karibuni wamekuwa wakiucheza mpira hivyo.

Mfumo wa 3-4-2-1 ina maana viungo wawili walioko wanne wanakaba mmoja ana shambulia na wote wanajenga nafasi kuanzia nyuma.


Kombe la dunia /uchambuzi na Prosper Bartholomew.

Simu:+255716243875.

Barua pepe:barthaprosper@gmail.com


Maoni