TUZO ZA MO SIMBA AWARDS ZAPOKELEWA NA WANAMSIMBAZI

Mo simba awards iliyofanyika leo usiku huku Raisi mstaafu wa awamu ya pili Mheshimiwa Hassan Mwinyi akihudhuria na pamoja na muwekezaji klabuni hapo na shabiki mkubwa Mohhamed Dewji,Joseph Haule mbunge wa Morogoro almaarufu kama Profesa J, Edo kumwebe na Mwana FA katika hafla hiyo


Tuzo hizo zikigawiwa kwa wachezaji waliofanya vyema wakiwa na Simba msimu huu wa 2017-18 ulioisha huku tuzo ya kipa bora wa msimu ikimuendea Aish Manula bila ubishi aliyetua klabuni hapo mwanzo wa msimu huu ulioisha.

Mshambuliaji bora aliyewapiku John bocco pamoja na Mavugo katika kinyanganyiro hicho ni Mganda Emanuel okwi aliyepachika kimiani jumla ya mabao 20 msimu huu akitwaa tuzo ya mfungaji bora wa ligi pia.

Na kwa upande wa mabeki au walinzi imemuendea Erasto Nyoni akiwaacha mbali kina Mkwansi na wenzake.

Katika nafasi ya kiungo ilimuendea mwendesha timu Ramadhan Kichuya aliyekuwa mwokozi wa msimbazi mambo yalipokwenda kombo.

Tuzo ya mchezaji bora wa mwaka imemuendea Mshambuliaji John Bocco huku akiwapiku nyota wote klabuni hapo huku akipata pia goli bora la mwaka la Simba.



Habari na Posi Figo Jr.

Simu:+255629436561.


Maoni