Kiungo Mfaransa Thomas Lemar anatarajiwa kujiunga na klabu ya Atletico Madrid baada ya klabu hiyo kufikia makubaliano ya awali na klabu ya Monaco ya Ufaransa.
Mchezaji huyo kwa sasa yuko na kikosi cha Ufaransa akijiweka vizuri katika fainali za kombe la dunia zitakazorindima nchini Urusi baadaye wiki hii.
Lemar 22 alikuwa anawidwa kama lulu na klabu mbalimbali barani Ulaya lakini tovuti ya Atletico Madrid ilitoa taarifa kuhusu makubaliano hayo baina ya klabu hizo mbili.
Akiwa bado ana miaka 22 tayari ashaitumikia timu ya taifa ya Ufaransa katika michezo 12 na amefunga mara tatu mchezo wake wa kwanza na jezi ya Ufaransa ilikuwa dhidi ya Ivory coast.
Habari na Prosper Barthalomew.
Maoni