Klabu ya Real Madrid inafanya mkataba wa awali na Roma kuhusu usajili wa kipa wao Allison anayetarajia kuidakia timu ya taifa ya Brazili,Roma itafaidika kwa kiasi cha pauni 43.7 milioni sawa na Euro 50 milioni huku Liverpool hana nguvu ya kuzuia mkataba na Real Madrid
Arsenal ya ligi kuu Uingereza inataka kumsajili kipa mjerumani anayekipigia klabu ya Bayern Levekusen Bernd Leno 26 katika dirisha hili la kiangazi haswa kama mrithi sahihi wa kipa namba moja Petr Cech anayeonekana amechoka baada ya kutimiza miaka 36 mwezi wa tano mwaka huu.
Klabu ya Aston villa itakuwa ngumu kukazia kuwauza Wachezaji wake baada ya klabu kuwa katika ushukaji wa uchumi Spurs wameweka ofa ya pauni 15 millioni kwa kiungo wao Jack Grealish.
Arsenal pia inafanya uwezekano wa kukamilisha usajili wa kiungo wa Sampodoria ya Italia Luccas Torreira ambapo kiungo huyo anekuwa akihusishwa kwa muda gunners hao London.
West ham imejitahathiti kuharibu kunako Swansea kwa kuwataka kwa pamoja mlinzi wa kati Alfie Mawson pamoja na mlinda mlango Lukas Fabiaski kocha wa washika nyundo Manuel Pelegrino hataki mzaa anataka kukisuka kikosi hicho kwani alifanya hivyo alivyokuwa na City.
Kiungo na winga wa Manchester United Antony Martial anahusishwa na kuondoka klabuni hapo baada ya wakala wake kukaririwa anafunguka kuhusu mteja wake Manchester united walikuja juu na kusema wana mpango thabiti na mchezaji wao huku Spurs na blues wana ngangania sahihi yake kwa muda mrefu sasa.
Winga na Mshambuliaji wa Ufaransa Antonio Graizeman alikiri kutumia mtandao wake wa Twitter ataendelea kusalia klabuni Atletico Madrid kabda ajaposti ujumbe huo alikiri kutumia makala ya dakika chache iliyorushwa kupitia chombo cha habari cha ufaransa alikuwa anahusishwa na klabu ya Barcelona licha ya msimu uliopita mwaka 2017 katika majira ya kiangazi alihusishwa sana na klabu ya Manchester United kabda ajaamua kusalia klabuni hapo
Klabu ya Chelsea imeitupilia mbali dau liloletwa na Arsenal wanaotaka kumsajili beki mbrazili David Luiz amekuwa akikosa namba katika kikosi cha kwanza baada ya kusemekana alimkosoa kocha Antonio Conte katika mchezo wa ligi ya mabigwa Ulaya dhidi ya Roma.
Klabu za Arsenal,Everton na West ham wanataka kumsajili Mario Gotze katika dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi.
Habari na Prosper Barthalomew
Simu:+255716243875
Maoni