Mlinda mlango wa Roma Allson Becker amesisitiza anafuraha na klabu yake ya Roma licha ya kumezewa mate na Liverpool (Tele Radio sterio)
PSG wanatamani saini ya mkata umeme wa Chelsea na Ufaransa N'golo Kante 27 na wamefanya mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo (Paris United)
pichani:Kante akiwa anausukuma mpira katika mchezo wa fainali ya FA msimu ulioisha pembezoni Rashford.
Inter Milan wanatamani saini ya beki Muitaliano Davide Zapacosta wa Chelsea amekuwa akipata mda mchache wa kuonesha makali yake darajani (totosport)
Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales atasalia klabuni hapo mpaka kocha mpya atakapotangazwa licha ya Manchester united kuisaka kwa udhi na uvumba sahihi yake (independent)
Pichani:Gareth Bale akiwa anafunga bao katika fainali ya ligi ya mabigwa ulaya msimu ulioisha dhidi ya Liverpool.
Bigwa wa Italia Juventus ana imani ya kupata sahihi ya kiungo aliyeko chini ya kivuli cha Arsenal Jack Wilshere 26 kuhusu (Football London)
Chelsea wana dili na Roma kuhusu kiungo Alesadro Florenzi ambaye ana miaka 27 dili hilo linaweza likafanyika siku za hivi karibuni (Gazzete dello sport)
Leonardo Bonnuci 31 ana sema hajali chochote akiwa na jezi ya Milan amesema anafuraha licha yakuhusishwa na Manchester united.(checkupblitz)
Real Madrid wameandaa kitita cha pauni 132 milioni kwa kiungo Mseribia wa Lazio SergieJ Milikovac-Savic 23 licha ya Manchester united kumuandama kwa muda mrefu (ill Messagero)
Pichani:Savic akipasha misuli kuelekea kombe la Dunia Urusi.
Habari na Prosper Barthalomew.
Simu:+255716243875.
Baruapepe:barthaprosper@gmail.com.
Maoni