SergeJ Milkojevic-Savic amekiri ana nia ya kujiunga sehemu yoyote lakini atarudi Roma maana bado ana mkataba na Lazio na atafutahia kuchezea huko msimu ujao lakini huku amekiri atapumzika kabda ajafanya maamuzi pengine. Amehusishwa na klabu za Manchester United,Juventus,na Real Madrid.
klabu ya Manchester United imedaiwa inataka kufanya usajili wa mlinda mlango namba tatu baada ya De gea,Romero nae ni Muingereza Lee Grant.
Everton wamefungulia jicho kwa mshambuliaji wa Croatia Ante Rebic baada ya kiwango safi anachoonesha katika kombe la dunia.
Arsenal imefuatiia kwa karibu kupata saini ya Hector Herrera ambaye yuko na Mexico katika michuano ya kombe la dunia.
Wayne Rooney anatarajia kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu na klabu ya DC United ya ligi kuu Marekani na amethibitisha kuwepo safarini.
Klabu za Southampton na Everton zinamsaka kwa udhi na uvumba saini ya Vestegard 25 ambaye anakipigia klabu ya Borrusia Monchegdbach na ni beki wa timu ya taifa ya Dernmarki.
Kocha Roy Hodgson wa Crystal palace amepewa ofa ya mkataba mmoja zaidi ya kuitumikia klabu hiyo baada ya kufanikisha kuisalisha timu hiyo katika ligi , kwa sasa kama ataikubali ofa hiyo atakuwa na mkataba huo mpaka mwaka 2020.
klabu ya Juventus imemsaini beki Joao Concelo kutokea Valencia kwa dau la pauni 35.3 milioni.
Tetesi na Prosper Bartholomew.
Simu:+255716243875.
Barua pepe: barthaprosper@gmail.com.
Maoni