TAARIFA ZA USAJILI NA TETESI ZA SOKA JUMANNE

Klabu ya Barcelona imeamua kuelekeza nguvu kubwa kwa kiungo Mbosnia na Harzegovinia Mirael Pjanic baada ya kumkosa Antonie Graizeman huku wakimuangalia kwa karibu mshambuliaji wa Manchester city Gabriel Jesus.


Mouroune Fellaini amedai atasema kuhusu hatima yake ya maisha yake ya soka julai mosi mkataba wake utakapoingia mwishoni na klabu ya Manchester United.



Wakala wa Mateo Darmian amekutana na Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Juventus kuangalia kama kuna uwezekano wa kumsajili kutoka Manchester United.


Inter Milan wamekamilisha kumsajili mbeligiji Radja Naiglolan kutokea Roma kwa dau la pauni 21 milioni.


Inasemekana Edern Hazard amekataa ofa ya pauni 340,000 kama mshaara kwa wiki kutoka kwa Chelsea ili kurahisha dili lake la kujiunga na klabu ya Real Madrid ambayo inamsaka kwa muda sasa.

Kiungo Muargentina Javier Pastore yuko Italia mjini Roma kukamilisha dili la miaka minne na klabu ya Roma huku akitarajia kusaini mkataba mda wowote kuanzia sasa,anatokea klabuni PSG.


Klabu ya PSG inayoshiriki ligi kuu Ufaransa imetoa ofa kwa Manchester United ya kumchukua Paul Pogba kwa kuwapa Muitaliano Marco Verrati na fedha kadhaa.


Manchester United imeingia nayo kwenye mbio za kumuwania beki wa Uruguayi Diego Godin amekuwa bora zaidi na Atletico Madrid ya Hispania na amebakia na mkataba wa mwaka mmoja tu atapatikana kwa dau la pauni 18 milioni.


Manchester United wanataka saini ya Mcroatia Mateo Kovacic ambaye anataka timu itakayompa mda mrefu wa kucheza,anataka kuondoka Santiago Bernabeu kipindi hiki cha majira ya kiangazi.


Sevilla wamepiga kufuli kwa kiungo wao Muargentina Ever Banega kwamba si wa kuuzwa kipindi hiki cha majira ya kiangazi wakiwa wanakata tumaini la kocha wa Arsenal Unai Enermy ambaye alifanya nae kazi klabuni hapo.

Chelsea hawataki kabisa kusikia suala la mauzo ya kiungo wao Ruben Lotfus-Cheek (22) lakini wataweza kumtoa kwa mkopo huku klabu za Crystal palace,Everton na West Ham zikileta urafiki kwa kiungo huyo.

klabu ya Ispiwich town imepata kumsaini kwa mkopo beki wa Chelsea Trevoh Cholobah kwa mkopo wa msimu mzima.

Klabu ya Sevilla inamtaka kumsaini nahodha wao wa zamani Vincent Ibbora kutoka walikomuuza Leicester city,tangia atue klabuni Leicester alitumika nusu msimu na baadhi ya michezo na klabu ya Sevilla inataka kurudisha huduma yake nchini Hispania.

USAJILI na Prosper Bartholomew.

Simu:+255716243875.

Barua pepe:barthaprosper@gmail.com

Maoni