TAARIFA ZA USAJILI NA TETESI ZA SOKA JUMATATU

Juventus wanaongoza njia ya  kumtwaa beki raia wa Uruguayi wa Atletico Madrid Diego Godin ambaye anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na atapatikana kwa pauni 18 milioni tu.



Klabu ya Inter Milan imethibitisha kupitia kocha wake Luciano Sppataeli  hawatataka kumuuza staa wake Maurio Icardi kwani ni mchezaji muhimu kwao.

Mkataba wa Fellaini unahisha ndani ya mwezi huu kukiwa na namba kubwa ya vilabu vinavyosaka saini yake ikiwa Arsenal ,vya vilabu vya uturuki.

Klabu ya Liverpool itafaa kuongeza zaidi pauni 10 milioni zaidi ya ofa ya kwanza kwa ajili ya kumtwaa kiungo Mfaransa Nabil Fekir.Hasa baada ya kufeli kumsajili kabda ya mwanzo wa kombe la  dunia na sasa wanabidi waanze mazungumzo na kiasi cha pauni milioni 62 kwa ajili ya kiungo huyo wa Lyon.


Newcastle wanaweza kumtwaa Mattie Ritchie kurudi Bournemouth ili waweze kumtwaa Josh King ambaye Rafa Benitez anamtaka kikosini hapo kwa ajili ya msimu ujao.

Jack Wilshire amepewa ofa na West ham United lakini hatataka kutua klabuni hapo kwa sababu amepewa mkataba wa mwaka mmoja tu huku kiungo wa miaka 26 hataki kusaini mkataba wa muda mfupi kiasi hicho,yuko bure sokoni.

Ripoti zinadai Marco Silva anataka kusafisha kikosi cha Everton kwa kuwauza mastaa wanne akiwamo Morgan Schneiderlin,Ashley Williams,Yonack Bolasie na Wayne Rooney na kuwaleta kikosini hapo Jack  Wilshire pamoja na Ruben Lotfus-Cheek.


Ripoti kutoka magazetini zinadai ya kuwa Sarri anaweza tua london mda wowote kukamilisha dili la kuwa kocha mpya wa kikosi cha blues huku akipewa mkataba wa miaka miwili na mkataba wa mwaka mmoja zaidi.

Inasemekana Unai Enermy kaanza mazungumzo ya kumvutia Muargentina Ever Benaga kikosini Arsenal.

West ham haitakata tamaa au kupotezea ndoto yao kuzama ndani ya maji ya kumtwaa kiungo mbrazil Filipe Anderson wa Lazio.West ham wanatarajia kutuma maskauti wao kufanya mazungumzo na Lazio wiki hii.

Watford wanataka kutoa pauni 10 milioni ili kumtwaa mlinda mlango Bern Forster kutoka West brom ambayo imeshuka daraja.


Tetesi za soka na Prosper Bartholomew.

Simu:+255716243875.

Barua pepe: barthaprosper@gmail.com


Maoni