Taarifa kutoka Italia zinasema Arsenal inasaka saini ya Mmoroco Medhi Benatia huku akiwa na miaka miwili katika mkataba wake wa sasa na Juventus pia Borrusia Dortmund anatamani saini ya beki huyo.
Juventus wanakaribia kumwaga kitita cha euro 38 milioni kwa Valencia kumchukua Joao Cancelo na huenda ata vipimo vya afya vikafanyika kesho.
Kutoka Italia ripoti zinadai Radja Naigglolan anaweza akajiunga na Inter Milan siku za karibuni huku ikidai vipimo vya afya viko karibuni.
Baada ya kukosa nafasi katika kombe la dunia katika kikosi cha Ufaransa Lucas Digne anataka kuondoka Barcelona katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi ili apate nafasi kubwa ya kucheza.
Roma imekamilisha usajili wa beki wa umri wa miaka 18 William Bianda ambaye ametoka lens.
Manchester United wameripotiwa kumuulizia Klyian Mpape ambaye huenda asijiunge na klabu ya PSG kutokana na FFP inayoikumbuka klabu hiyo,Manchester city pia imetamani saini yake.
Alvaro Morata ana husushwa kujiunga na klabu ya Dortmund huku Chelsea wakitamani kutumia nafasi hiyo kumnasa winga Mmarekani wa miaka 19 Christian Pulisc ambaye anaonekana lulu barani Ulaya.
Habari na Prosper Bartholomew.
Simu:+255716243875.
Barua pepe: barthaprosper@gmail.com.
Maoni