Lukas Fabiaski 33 amesajiliwa rasmi na klabu ya London ya West ham akitokea klabu ya Swansea City anatarajiwa kutua klabuni hapo rasmi baada ya kombe la dunia kufika tamati,ataitumikia klabu hiyo kwa kandarasi ya miaka mitatu.
Sinisa Mihlajlovic amefanya uamuzi mgumu wa kujiunga na kuwa kocha wa Sporting lisbon.
Ambapo mashabiki wamekuwa na vurugu mpaka kuwavamia wachezaji baada ya kukosa nafasi katika ligi ya mabigwa ulaya ,Wachezaji watano wamesitisha mikataba yao na klabu hiyo akiwemo Rui Patricio aliyejiunga na Wolverhampton jana akiwa bado na timu ya taifa ya Ureno.
Manchester United wamemuwekea dau la pauni 100 milioni kwa timu itakayotaka kumtwaa mshambuliaji mfaransa Antony Martial ambaye amehusishwa na vilabu vya Chelsea na Tottenham Hotspur.
Mshambuliaji raia wa Groatia Adrej Kramaric amewekewa dau la pauni 43.5 milioni na klabu ya Hoffenham huku Newcastle wamekuwa wanamfuatilia kwa muda mrefu.
Kiungo raia wa Australia Aaron Mooy anawidwa na klabu ya Everton na Southampton zote zikiwa tayari kutoa kiasi cha pauni 18 milioni.
Burnley wana mpango wa kumsaini tena Jay Rodriguez kutoka timu iliyoshuka daraja West Bromwich kwa ada ya pauni 20 milioni.
Klabu ya Crystal Palace imempa ofa Wilfred Zaha ya kusalia klabuni hapo na kuna kuvuna kitita cha pauni 120,000 kwa wiki.
Alexander Golovin amekuwa anawidwa na klabu nyingi barani ulaya sasa Arsenal imeanza kumyatia kipindi hiki kukiwa na taarifa ya kuwa ameshaanza kujifunza lugha ya kiingereza.
Habari na Prosper Bartholomew.
Simu:+255716243875
Maoni