TAARIFA ZA USAJILI NA TETESI ZA SOKA JUMATATU

Taarifa zinadai Real Madrid wako tayari kutoa ada ya euro 150 milioni kwa ajili ya mserbia SergeJ Milkojevic-Savic ambaye ni shabiki wao na anakipigia Lazio kwa sasa.


Joe Allen ameongeza mkataba na klabu ya Stoke city na ataendelea kuchezea Stoke city licha ya klabu hiyo kushuka daraja msimu huu.

Taatifa kutoka Ureno zinasema kocha mpya wa Arsenal Unai Emery anaitaji huduma ya mchezaji wa Porto Brahimi na huduma yake itawagharimu kiasi cha euro 30 milioni.

Ac Milan haina hamu ya kumuunza mshambuliaji wake Adre Silva katika majira haya ya kiangazi na wamemuambia wakala wake Mino Raiola na kama litatokea hilo euro 35 milioni zitamuusu mhitaji huduma.

Hazard amehusishwa ana hamu ya kujiunga na mabigwa mara tatu mfululizo wa ligi ya mabigwa ulaya Real Madrid akidai wafanye mchakato kama wataitaji huduma yake.


Habari na Prosper Bartholomew.

simu:255716243875.


Maoni