TAARIFA ZA USAJILI NA TETESI ZA SOKA

Nafasi ya Gareth Bale ndani ya klabu ya Real Madrid inazidi kupewa nafasi kubwa baada ya kocha mpya Julen lopertegui kuwa anajua kuongea kiingereza ambapo Zidane alikuwa hawezi.

Klabu ya West ham ina imani ya kumpata kiungo mwingereza Jack Wilshere ambaye mkataba wake unaelekea mwishoni mwezi huu wa juni na apewi nafasi kubwa kutosaini mkataba mpya klabuni Arsenal.

Manchester United wanataka kuweka kizuizi cha pauni 75 milioni kwa mshambuliaji wao Antony  Martial asiye na furaha klabuni hapo ambaye anawidwa na Chelsea na Spurs.

Michail Antonio anataka kuondoka West ham huku akihusishwa na klabu ya Crystal Palace amekuwa nguzo muhimu klabuni West ham kwa miaka ya hivi karibuni.

Habari na  Prosper Bartholomew.

simu:255716243875

Maoni