TAARIFA ZA USAJILI NA TETESI ZA SOKA JUMAMOSI

Taarifa zinasema mlinda mlango wa kihspania David De gea amekubaliana na Manchester United mkataba wa miaka mitano kuachana na tetesi za kuwakimbia kwenda Real Madrid.

Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale amesema kuwa ana hamu ya kuendelea kufanya kazi chini ya kocha Julen Lopetegui kuliko kurudi ligi kuu uingereza.

Barcelona wamemisi huduma ya mbrazili Neymar Jr na wanaangalia uwezekano wa kumrudisha klabuni hapo tena aliondoka kwa dau la pauni 198 milioni kuniunga na PSG katika dirisha la majira ya kiangazi 2017.


Maurrizio Sarri yuko katika hatua za mwisho na klabu ya Napoli kwani bado ana mkataba licha ya kuwa Carlo Ancelloti kashachukua nafasi yake klabuni Wakala wake anamalizia na Napoli wikiendi hii huku mambo ya kumrithi Conte yakiwa njia panda.

Atletico Madrid wana hamu ya kuuboresha mkataba wa mlinda mlango wao Jan Oblack baada ya PSG,Real Madrid na Liverpool kuanza kuwa kinanganizi.

Spurs wanachungulia upepo wa Dortmund kwa kiungo mjerumani Mario Gotze 26 kama wataweza kungoa kwa pauni 16 milioni.

PSG wana imani ya kumsajilli mchafuaji N'golo Kante kutoka Chelsea.kwa dau la pauni 90 milioni kwa mafaransa huyo kurudi nyumbani.

Maoni