SIRI YA URUSI KAMCHINJA SAUDIA ARABIA

Urusi amewaonesha wengi waliodania kuwa yeye ni kibonde kuwa alikuwa anatania tu sasa kombe la dunia kashinda kwa mabao matano kwa sifuri nampa asilimia 45 mpaka 60 za kwenda raundi inayofuata kumbuka ukishinda michezo miwili katika kundi lako umefuzu raundi ya 16 bora.

Siri nyingi zimemsaidia Urusi ya kwanza ni uwepo wa mashabiki yaani uwenyeji wake umemsaidia sana kwani mashabiki mda wote walikuwa wanawapa moyo wachezaji amna mda uwanja ulikaa kimya  ikawapa wachezaji motisha wa kufanya vyema napenda kusema ya kuwa mashabiki ni mchezaji wa 12 ndani ya uwanja si walaumu saudia kwa hii siri ya kwanza kutoka kwangu kwani hawakuwa kwao.


Pichani:mashabiki wa Urusi wakishangilia kwa dhati timu ya taifa lao.

Siri ya pili ni ushambuliaji wa Urusi ulikuwa mwiba kama si mwangalizi mzuri utafikiri magoli talibahatika ukweli ni kuwa walijipanga na kutumia njia fulani ya hivi mshambuliaji akipata mpira kina Smolov na Dzyaba walikuwa wanatuliza mpira na kusukuma wenzao mbele ambao walikuwa wanatia kambani magoli yao goli ambalo halijapitia kwa mshambuliaji wa kati na kuwa goli ni goli la kwanza na la mwisho. Pengine hii njia ya ufungaji magoli ni kwa timu chache zinazojiamini maana unaweza kosa au kufanya uzembe utakaoigarimu au ukakosa sehemu ya kufunga,kingine mshambuliaji wa timu hii alikuwa anaibia pasi mbaya zikizokuwa zinapigwa na Saudia.Utagundua kutimia mbinu hizi Urusi amejikuta akipiga au akishambulia mara 13 na mwenzake akifanya 6 huku kati ya 13 zaidi ya nusu namaana 7 yalikuwa yamelenga goli.


pichani : Dzyaba akishangilia bao alilofunga baada ya kucheza dakika 1 na sekinde 29 na kujikuta na bao

Siri nyingine ni ukabaji au kazi ya ulinzi ilifanywa na timu nzima amna ambaye ilikuwa kazi yake kuanzia mshambuliaji wa kati wote walikaba kwa moyo mfano goli la pili lilitokanana na ukabaji uliofanywa ndani ya eneo la adui na kuipa Urusi bao na huku Smolov kapitisha mguu wake tena ndo maana Saudia hajapiga shuti lolote lilolenga goli.


Utimamu ndani ya mchezo ndo siri yao nyingine kubwa kocha wao alihakikisha timu inatulia ndani ya dakika 90 sjapata ona Urusi iliyokuwa imetulia ndani ya mchezo kama urusi ya leo walikuwa hawana haraka walijua ukicheza mpira ukiachana na kuufanya mpira ukuendeshe utapata ushindi angalia goli la pili la tatu la nne na la tano kweli kocha wetu kawafanya wakawa na utimamu.


pichani:Kocha wa Urusi akishangilia bao la Dzyaba.

Saudia nafikili wakiukosa utimamu huu ndani ya mchezo ndo labda ulikuwa ugonjwa wao wa leo.

Uchambuzi/kombe la Dunia na Prosper Barthalomew.

Simu:+255716243875



Maoni