SINEMA LAWA ZITO SASA SARRI ATANGAZA MSHAMBULIAJI WAKE CHELSEA

Kocha mtarajiwa wa Chelsea Maurizio Sarri amesema atataka kuungana na mshambuliaji wake Dries Martens wa Napoli atakapotangazwa kocha wa Chelsea.

Chelsea wanakaribia kumteua Maurizio Sarri kama kocha wao mpya kurithi mikopa ya Antonio Conte ambaye bado ajatimuliwa na klabu hiyo.

Maurizio Sarri amewaambia marafiki wake atataka kuungana na mshambuliaji huyo aliyefunga takribani mabao 22 katika klabu yake ya Napoli msimu uliopita na huku akifunga goli la kwanza la ubeligiji katika kombe la dunia,Sarri pia atakapojiunga na klabu ya  chelsea inatarajiwa kutua kwa kiungo wa Nice Jean Michael Sarri.

Conte amejitahidi kuomba kusajiliwa kwa mshambuliaji huyu wa ubeligiji kwa misimu miwili iliyopita lakini klabu ya chelsea ilisema ni mzee na ni ghali kupatikana.Na ada ya kumnunulia katika mkataba wake ni pauni 24.5 milioni na hiyo inaweza ikaleta ugumu kwani klabu za China,PSG na Borrusia Dortmund wanahitaji huduma.


Habari na Prosper Bartholomew.

Simu:+255716243875.

Barua pepe: barthaprosper@gmail.com



Maoni