SALAH NA RAMOS MAMBO YAWA MAZITO

Staa wa Misri Mohhammed Salah ameshangaza wengi baada ya kusema atakaa amsamee Sergio Ramos kwa alichomfanyia.

Ramos nahodha wa Real Madrid alimchezea rafu mbaya Salah ambayo ilichangia kutolewa nje kwa staa wa Liverpool katika pambano la fainali ya ligi ya mabigwa ulaya ambapo Liverpool ililala kwa bao tatu kwa moja.

Pichani:Salah akitolewa nje baada ya kuumia katika fainali ya ligi ya mabigwa ulaya mwezi uliopita.

Ramos alikiri ya kuwa alimtumia ujumbe wa kumtia moyo haswa nafasi yake ya ushiriki wa kombe la dunia ilikuwa mashakani.

Salah amejibu mapigo kwa kusema ana mawasiliano ya kuambiana sawa na Mhispaniola huyo akiwa anaiambia gazeti la Marca la nchini Hispania.

"Alituma ujumbe lakini sikumwambia ni sawa "alisisitiza Salah.

:Kwa ajili ya picha kali na graphics disining usikumbwe na tatizo wasiliana na moja ya wakali hawa 0692344163 NBA VISUALS:

"Labda maoni yangu ni hivi aliyeweza kukufanya ulie , anawezaje kukufanya ukacheka labda angeniuliza nikoje naweza nikaenda kombe la Dunia? Si vinginevyo" staa huyo na mchezaji na mfungaji bora wa ligi kuu Uingereza alisema 

Habari na Prosper Barthalomew

simu:+255716243875.

Barua pepe:barthaprosper@gmail.com

Maoni