Ronaldo ana tamaa ya kufikisha rekodi za watanguliaji wake na kuzivunja na anajiamini yeye ni bora zaidi ya mpinzani wake na aogopi mashabiki bali ana fanya waache kumzomea na kadhalika.
Unaweza usiwe unampenda lakini kazi yake itakuvutia ukilinganisha na mchezaji mwingine,ana dhana kichwani mwake yeye bado ni mshindani tu.
Na miaka 33 bado anataka kuifuta rekodi ya Eusebio ya kuongoza magoli mengi katika kombe la dunia katika taifa la Ureno jumla magoli 9 bado mawili aifute rekodi hiyo.
Ashawai kuulizwa unadhani je wewe na Leo Messi nani bora watu wanadai yeye ni bora alichokijibu nilikipenda na siku zote mshindani anabidi awe hivyo alisema naheshimu maoni ya watu lakini kwangu mimi ni bora zaidi yake.Alisema hayo akiwa anatwaa ballorn d'or mwishoni mwa mwezi decemba.
Katika timu yake ya taifa eneo la ulinzi Rui Patricio na Pepe wana ongoza timu yeye ana hitaji mipira yote na Ureno hawataki kufunga kama mpira ujapitia kwa mshambuliaji wao ambaye wana muona kama ni moto wa kuotea mbali.
Ndani ya boksi ni msumbuaji mtafuataji na mshambuliaji na anavifanya vyote idadi ndogo ya nafasi anazozipata zinalisa watu katika nafasi nne alizozipata juzi katika mchezo dhidi ya Hispania basi tatu ziliingia ndani.
Katika kombe la dunia ashapiga magoli manne na huku akiweka rekodi ya mfungaji bora wa muda wote barani ulaya kwa timu za taifa baada ya kufikisha magoli 85.
Si kichwa,mguu wa kushoto,kulia,tumbo,paja,kisigino kila sehemu ya kiungo chake inawasha ikufunge kwangu ni mshambuliaji hatari kutokea na sasa ni mshambuliaji bora ulimwenguni.
Kombe la dunia/uchambuzi na Prosper Bartholomew.
Simu:+255716243875.
Barua pepe:barthaprosper@gmail.com
Maoni