PSG YAKALIA MOTO MKALI

Klabu ya PSG inayoshiriki ligi kuu Ufaransa maarufu kama ligue 1 wanatakiwa kuwauza baadhi ya wachezaji wake kwa kiwango kisichozidi milioni 60 euro sawa sawa na pauni 52.9 milioni kutokana na ukiukwaji wa sheria za usajili sokoni katika dirisha lilopita la majira ya kiangazi.

Klabu hiyo ilikiuka sheria zilizowekwa na FFP mwaka 2013 katika uanzishwaji wake  na imewekwa chini ya uangalizi maalumu na chama hicho huku shirikisho la soka barani Ulaya UEFA wakifanya uchunguzi mkali ndani ya klabu hiyo tangu mwezi septemba mwaka jana.

Haya yalitokea baada ya klabu hii kumsajili Mbrazili Neymar Jr kutokea Barcelona kwa pauni 198 milioni wakivunja rekodi ya usajili katika soko la wachezaji duniani.


Hata hivyo walimchukua kwa mkopo Klyian Mpape kutoka Monaco kukiwa na kifungu cha kumsajili moja kwa moja cha kiasi cha pauni 165.7 milioni katika majira haya ya kiangazi.Hata hivyo bado wajafikiana na klabu ya Monaco.

Habari na Prosper Barthalomew.

Maoni