Panama ni nchi ndogo ya watu wa hali ya kawaida tu. Kihistoria ya soka Panama ni nchi yenye heshima ya kawaida katika ulimwengu wa soka. Panama ni nchi ya watu wachapakazi, nchi iliyojaa vijana ambao wanaonekana kutafuta historia nzuri katika mchezo huu wa mpira wa miguu.
Panama ni inchi ambayo kwa sensa yao ya mwaka 2015 inaonesha kuwa na na watu wasiopungua 3,336,000. Kwa hesabu za haraka, panama 15 zinaunda Tanzania moja. Lakini kwa uchache wao huo na shirikisho lao la soka nchini panama wameweza kusaka vipaji vya kuibua timu hio ili kuweza kuweka heshima katika mchezo wa soka ulimwenguni.
Timu hii ilicheza mchezo wake wa kimataifa wa kwanza na kushinda kushinda magoli 3-1 mwaka 1938 dhidi ya Venezuela. Tokea hapo Watu wa Panama waliona Nuru na waliamini kwamba ipo siku itaweza kukaa katika chungu kimoja na Timu za mataifa makubwa kama Uingereza, Argentina na Mengine mengi.
Kwa kujikokota huko kimpira Panama iliwahi kushika nafasi ya 29 katika viwango vya fifa mwaka 2014, na baadae kushuka na sasa ivi ipo nafasi ya 55 katika viwango vya ubora wa soka duniani.
Leo Hii Panama imeweza kushiriki katika kombe la dunia kwa mara ya kwanza na unaposoma makala hii, tayar wameshatua nchini russia kwa ajili ya kuendelea kutengeneza jina zuri la nchi hio kwa upande wa soka. Ipo kundi moja na Ubelgiji, Uingereza na Tunisia. Katika kundi hio wengi wanaona kama panama anaweza kuwa bonde la utelezi. Lakini vijana hao Chini ya kocha Hernando Dario Gomez wanaamini kwamba wataishangaza Dunia katika michuano hio huko Urusi
Bado siku moja na masaa machache, Mashabiki wa Soka watashuhudia Maajabu katika michuano ya mwaka huu
Kombe la Dunia na:Rugambwa(infantino)
Simu:0629546461.
Maoni