NEYMAR JR ATEMA YAKE KUZIBA MIDOMO YA WENGI

Neymar ni miongoni mwa mastaa wanaotarajiwa kufanya mambo makubwa ndani ya Kombe la dunia huku Ronaldo wa Ureno na Messi wa Argentina wakiwa washatuonesha yao huku akikiri ya kuwa chake cha muhimu ni kushinda ubigwa wa dunia wala si ballon 'd or.

PICHANI:Neymar akiwa mazoezini jana.

Staa huyu wa kibrazili alikosa baadhi ya michezo ndani ya klabu yake ya PSG ya Ufaransa licha ya kuwa mchezaji bora wa ligi kuu hiyo baada ya kuwa majeruhi na sasa anaonekana yupo fiti kuanza kutimua vumbi huko Urusi huku macho mengi yakimuekekea leo dhidi ya Uswisi.


PICHANI:wachezaji wa Brazili na Neymar

"Sitaki kuwa bora duniani bali nataka kutwaa taji hili "alisema Neymar 

"Niko tayari kufanya kile kinachoweza kusaidia kutwaa taji hili na kuonesha kiwango changu bora "

Aliongezea mchezaji huyo ghali zaidi duniani.

"Nitaendelea kujitahidi kuwa kati ya bora "

Alisema hayo wakati anajiandaa kuanza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Uswinzi leo jioni .

Kombe la  Dunia na Prosper Bartholomew.

Simu:+255716243875





Maoni