MESSI: TUKO KAMA TIMU NYINGINE

Nadhodha wa Argentina Lionel Messi imembidi aitetea timu yake baada ya mashabiki wengi wa soka ulimwenguni kuitoa katika ramani za timu ambazo zinaweza twaa taji hilo nchini Urusi.

pichani:Lionel Messi akipasha misuli moja ya maandalizi ya kombe la Dunia

Argentina ilitinga hatua ya fainali msimu pale Brazil na kuambulia kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa ujerumani katika mda wa nyongeza yaani baada ya kufika tamati ya dakika 90.

Mshambuliaji huyo wa Barcelona atashiriki mara ya tatu michuano hii akiwa na mabao 5 tu licha ya kuwa mwanasoka bora wa dunia mara 5.

Alinukuliwa akisema wachezaji wote wana vipaji vikubwa na jitihada binafsi huku akijinasibu kuwa hawafikirii mizozo iliyoko na wana fikiria tu taji hilo huku akisema timu inapambana.

Aliongeza ya kuwa ana imani ya kutwaa taji hilo kipindi huku licha ya kupoteza wafuasi wengi kutokana na migogoro ndani ya timu hiyo.

Watapata hudumu ya mshindi mara mbili wa copa Amerika kocha Jeorge Sampaoli atakayekuwa anaongoza benchi la ufundi na wana vipaji vikubwa vinavyotesa barani ulaya kama Di Maria,Aquero,Otamendi na wengineo wengi.


Pichani:moja ya safari za hivi karibuni za timu ya taifa ya Argentina.

Kombe la Dunia na : Prosper Barthalomew.

Simu:+255716243875.

Baruapepe:barthaprosper@gmail.com


Maoni