Hary Kane na Alexander Mitrovic wote wamelalamika walivutwa ndani ya boksi na mfumo hukufanya chochote malalamiko haya yaliwekwa wazi katika michezo ya makundi iliyokamilika jana.
"Pengine unaweza sifu kwa sababu kuna matukio ghafla yamepotea" Alisema mwenyekiti wa chama cha marefa Pierluiga Collina.
Jumla ya matukio 335 yaliangaliwa katika raundi za makundi huku 14 marefa wakienda kuziangalia wenyewe .
Waamuzi wanasema jumla ya matukio ya wastani wa asilimia 95 yalifanywa kihalali bila matumizi ya VAR ambayo imetumika kwa mara ya kwanza katika mashindano ya dunia hapa Urusi. Wamesema VAR imefanya kazi kwa usawa wa asilimia 99.3.
"Tumesisitiza na tumekuwa tukiwaeleza VAR haina maana ya usawa kabisa bado kutaendelea kuwa na makosa pamoja na kutotafsiri kama inavyotakiwa"
"Nadhani 99.3% ni karibu na usawa"
Alisema Collina.
kombe la dunia na Prosper Bartholomew.
Simu:+255716243875.
Barua pepe: barthaprosper@gmail.com.
Maoni