Klabu ya Olympic Lyon wameamua kusitisha mazunguzo na klabu ya Liverpool katika suala la kumsajili kiungo mfaransa Nabir Fekir.
Klabu zote mbili zilikuwa katika mazungumzo yanayohusisha kiasi cha euro milioni 60 kwa kiungo mchezeshaji huyo.
Wawakilishi wa Lyon wametoa taarifa ya kusema wanambakisha nahodha wao Fekir 24 kwa kudai makubaliano yanesitishwa ghafla na wanatarajia kupata huduma ya kiungo huyo msimu ujao.
Pichani: Nabir Fekir akiucheza mpira akiwa Lyon
Kiungo huyo amekuwa moja ya windo kubwa la Mjerumani Jurden Klopp katika kukipa nguvu na makali kikosi hicho kilichotinga fainali ya ulaya msimu huu na kulazwa kwa bao 3 kwa 1 na Real Madrid
Nabir Fekir anatarajia kupaa ndege baada ya kumaliza mchezo wa kirafiki na Marekani baadaye kuelekea Urusi.
Habari na :Prosper Barthalomew
Maoni