Leo ni tarehe 14. Siku ambayo ilipangwa miaka michache iliyopita kwamba ndo Mashindano kilele ya soka duniani yataanza huko urusi. Urusi ni nchi ambayo historia yake kimpira ni ya kawaida sana na hata timu yake katika michuano hii haiogipeshi wapinzani kivile. Lakini Fifa kazi yake ni kusambaza mpira duniani kote, kazi ya pili kuu ya fifa ni kuhakikisha mpira ni mchezo ambao unakutanisha watu mbali mbali wa desturi mbalimbali na kuwakutanisha kuwa wamoja na ndo maana michuano hii inafanyika nchini urusi ambamo mpaka saa hii, humo wapo wareno, wabrazil, wahispania, wamisri, watunisia na pia ndugu zetu wanigeria. Wote sasa ivi wapo ndani ya nchi moja kushuhudia michuano hio kama mashabiki wa soka.
Maandalizi ya kombe la dunia huko urusi yalianza takriban miaka 8 iliyopita. Urusi walipopata taarifa kwamba watakua wenyeji basi walijipanga vyema kwenye kila sekta. Viwanja vizuri, miundombinu bora ya usafiri na mawasiliano, hoteli za kisasa na pia kuimarisha ulinzi nchini humo.
Raisi wa urusi Putin, aliahidi hata kweny kampeni zake za uraisi kwamba hatalala mpaka aone michuano hio imeandaliwa na inafanyika vyema katika nchi yake. Aliyasema hayo kwa sababu yeye mwenyew anaelewa ukubwa wa kitu kama hiki na jinsi nchi itakavyofaidika katika kuandaa michuano hio. Warusi kipindi hiki watafaidika sana haswa kiuchumi kwa sababu ndo wakati ambao biashara kama zote zinakua na wateja wa uhakika, kwahio ni faida hata kwa nchi nzima kama wananchi wataweza kutumia fursa hii vyema.
Jumla ya Timu za mataifa yanayoshiriki ni 32. Ni mataifa mengi na jumla ni wachezaj 736 wako pale kila mtu akitaka kuonesha dunia kwamba anastahili kushiriki michuano hio. Je hizo nyasi huko urusi zitakua na hali gani kwanzia leo jioni.
Je! Mnakumbuka Utamu wa michuano hii. Mnakumbuka Bao la Robin Van Persie dhidi ya Spain 2014 bao ambalo lilipewa jina la THE FLYNG DUTCHMAN. Je! Mnakumbuka Bao la James Rodriguez dhidi ya Uruguay mwaka 2014.Je! Mnakumbuka uwezo wa Diego forlan na mpira mzito jabulani mwaka 2010. Utamu wa kombe hili hauna kifani na ni wa aina yake katika mchezo wa soka. Ukikosa kuangalia kombe hili la dunia mwaka huu utakosa mengi sana.
Pia katika matukio mbali mbali ya soka, kuna watu wapo wanapanga kubeba kiatu cha dhahabu kama alivyofanya Luarent Blanc mwaka 98. Thomas Muller anaonesha njaa yake ya kubeba kiatu hicho na kuendelea kufukuzia rekod ya mjeruman mwenzie Miroslav klose ya mabao 16 ya kombe la dunia. Huku nao wamsiri wameenda na rekodi yao ya kua na mchezaji mwenye umri mkubwa katika kombe hili ambae pia ni kipa na nahodha wa kikosi hicho Essam El Hadary miaka 45. Katika kombe hilo kuna mtu kama kylian Mbape yeye ana umri wa miaka 20 ni kama mtu na baba yake wanacheza katika michuano hii. Hizo zote ni burudani za kombe la dunia. Nikome kabisa kuendelea kumaliza utamu huo wakat bado masaa tu pale russia panukie mpaka dunia nzima tunuse. Tukiwa sambamba na fifa wote tunasema MY GAME IS FAIR PLAY
Kombe la dunia 2018 Russia
Kombe la Dunia na Rugambwa(infantino)
Simu: 0629546461
Maoni