Klabu mbalimbali nchini Uingereza zilipokutana katika kikao kipindi hiki cha majira ya kiangazi katika mkutano wa EFL wamepiga kura kupitisha sheria mbalimbali na kuziangusha nyingine zitakazotumika msimu ujao katika kombe la ligi.
Mathalani mda wa nyongeza (extra-time) baada ya suluhu umefutwa rasmi ikiwa ina maana timu zikitoka suluhu watapiga mikwaju ya penati moja kwa moja.
Pia klabu nyingi zilisapoti kutokewa kwa mda wa nyongeza wa dakika 30 huku wakitoa mchango mkubwa wa upigaji wa penati baada ya dakika 90 za mda wa kawaida.
Wakati huo huo wamepitisha kurudish
Pichani:wachezaji wa Manchester city wakisherekea ubigwa msimu ulioisha 2017-2018
wa mfumo wa zamani wa upigaji penati na kuachana na mfumo wa ABBA uliotumika msimu wa 2017-2018.
Pia EFL walithibitisha utumiaji wa msaada wa video katika utoaji maamuzi (VAR ) kwa michezo yote msimu ujao itakayopigwa katika viwanja vya ligi kuu uingereza alimaarufu kama (EPL)
Habari na:Prosper Barthalomew.
Simu:+255716243875.
barua pepe:barthaprosper@gmail.com
Maoni